Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 17, 2011

RAPA MACHACHARI WA TWANGA DIOUF KUTOKA KIFUNGONI J'4


MSAFIRI Said almaarufu kwa jina la 'Diouf' anayejiita Babu wa Loliondo na mwingi wa ma a.ka kesho Jumanne anatarajiwa kumaliza adhabu yake ya onyo alilopewa na Meneja wa Bendi ya Twanga Martin Sospeter ambayo alipewa Ijumaa iliyopita kufuatia kufanya uzembe kazini.


Habari hiyo imethibitishwa usiku huu kwa njia ya simu na Sospeter kwamba Kesho Diouf anatakiwa kuripoti kazini baada ya kumpatia onyo kali na kutomruhusu kupanda stejini Ijumaa iliyopita wakati bendi ya Twanga ilipotumbuiza kwenye viwanja vya hoteli ya Lamada iliyopo Ilala Jijini Dar es Salaam.

"Kesho Diouf anatakiwa kuripoti kazini hivyo tunatumaini kila kitu kitakuwa sawa na yeye atarudi kazini akiwa na ari mpya"alisema.http://bongoweekend.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...