Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 3, 2011

Mshindi Pool vyuo vikuu kulamba milioni mbiliNaMwandishi Wetu


WADHAMINI wa michuano ya mchezo wa pool kwa vyuo vya elimu ya juu, Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) wametangaza zawadi kwa washindi ambapo bingwa atajinyakulia Shilingi milioni mbili pamoja na kikombe.

Michuano hiyo inayojulikana kama 'Higher Learning Safari Pool Competition' yatafanyika katika mikoa ya Dar es salaam,Morogoro,Dodoma,Mwanza,Iringa,Mbeya, Kilimanjaro na Arusha ambapo fainal za kitaifa zitafanyika mkoa wa Dodoma


Kuhusu zawadi alisema kwa mwaka huu katika ngazi ya mkoa kitaifa jimla ya milioni kumi na nane na laki sita zitatolewa fedha hizo na zawadi nyingine zitafanikisha kuwasaidi wanavyuo kuweza kupata namna ya kuongeza ufanisi wa kimasomo lakini pia kuweza kupata changamoto ya kukutana miongoni mwa wanavyuo wa chuo kimoja na kingine

Alisema zawadi za mikoa mchanganuo wake ni mshindi wa kwanza sh.500,000.00 mshindi wa pili sh.300,000.00 mshindi wa tatu sh.200,000.00 na wa nne sh.50,000.00 na wachezaji mmoja mmoja mshindi ni laki moja

Ngazi ya taifa ni mshindi ni milioni mbili wa pili milioni na laki tano na mshindi wa tatu milioni na laki tatu mshindi wa nne milioni moja ambapo kwa wachezaji mmoja mmoja mshindi ni laki tatu wa pili laki mbili na watatu laki na nusu alisema shelukindo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...