Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 24, 2011

MISS LINDI 2011 KUPATIKANA JUNI 4


Na Dina Ismail


SHINDANO la kumtafuta Miss Lindi mwaka 2011 linatarajiwa kufanyika juni 4 mwaka huu katika kumbi wa hoteli ya Lindi Oceanic mkoani Lindi,imefahamika.
Mratibu wa shindano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Alliance Entertainment Shah Ramadhan alisema mpaka sasa warembo tisa wamejitokeza kwa ajili ya kushiriki shindano hilo na kusema kuwa milango bado ipo wazi kwa wasichana wenye sifa kujitokeza.
Alisema warembo watakaoshiriki wanatarajiwa kuanza kujinoa Mei 29 katika ukumbi huo huku mkufunzi aliyebobea katika masuala hayo Caroline Zayumba akitarajiwa kuendesha zoezi hilo.
.”Kwa kweli tumejipanga kuhakikisha tunatoa mrembo ambaye atarudisha hadhi ya mkoa wa Lindi kama miaka iliyopita, warembo tulionao wote ni bomba, pia tunaomba wadhamini wajitokeze kwa wingi kutusaidia”, Alisema.
Mratibu huyo alisema mpaka sasa makampuni yaliyojitokeza kudhamini ni pamoja na Vodacom, Ndanda Spring Water, Muhsin General Enteroprises, Live Trading Center, Pride Fm na Lindi Oceanic hotel.
Taji la Miss Lindi linashikiliwa na Mary Adam pichani kushoto.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...