Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, May 2, 2011

UDOM wang’ra uzinduzi tamasha la ‘Excel with Grand Malt’
Na Mwandishi wetu, Dodoma

Kikundi cha muziki wa dansi cha Dancing Revolution cha Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), juzi kiling’ra katika tamasha la uzinduzi wa promosheni ya Excel with Grand Malt lililofanyika katika viwanja vya Central mjini Dodoma.

Kikundi hicho ambacho kinaundwa na wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dodoma kilivuta hisia za umati mkubwa uliohudhuria katika viwanja hivyo kutokana na umahiri wake wa kucheza nyimbo mchanganyiko zikiwemo nyimbo za zamani maarufu kama zilipendwa.

Excel with Grand Malt ni promosheni inayoendeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake ambacho hakina kilevi cha Grand Malt, yenye lengo la kutoa tuzo za aina mbalimbali kwa wanafunzi kutoka vyuo vya elimu ya juu hapa nchini.

UDOM ni mojawapo ya vyuo 20 vya elimu ya juu vinavyoshindania tuzo ya Excel with Grand Malt. Washindi watajinyakulia zawadi mbalimbali ambapo zawadi kubwa itakuwa hundi ya kununulia vitabu yenye thamani ya shilingi laki nne. Tuzo hizo zinashindaniwa katika makundi manne ambayo ni utamaduni na burudani, huduma za jamii na mazingira, ugunduzi na kipaji maalum.

Akiongea katika Tamasha hilo ambalo lilitawaliwa na michezo mbalimbali kama vile soka na mpira wa wavu, Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt Consolata Adam alisema aliwashurukuru wanafunzi wa UDOM kwa kutoa burudani ya kusisimua.

“Tuna amini kuwa kwa burudani mliyoitoa hapa huenda tuzo mojawapo ikaja kwenu kwasababu burudani mlioyoitoa hapa imeonyesha ubunifu kwa kiasi Fulani, ongereni sana nawashauri mtumie Grand Malta kinywaji ambacho hakina kilevi, Alisema.

Vyuo vinavyoshiriki katika kinyang’anyiro cha tuzo hizo ni Chuo cha Mzumbe, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Elimu ya Biashara, Taasisi ya Jamii.

Vingine ni Chuo Kikuu Cha Elimu ya Elimu (DUCE), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Elimu Mkwawa na Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...