Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, August 8, 2011

Serikali yaboresha miundo mbinu ya ufundishaji katika Vyuo vikuu nchini- Dkt Kawambwa


Na Tiganya Vincent, Dodoma

Waziri wa Elimu Dkt Jumanne Shukuru Kawambwa alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Nne imeandaa Mpango wa Elimu Juu unaolenga kuboresha mapungufu yaliyojitokeza huko nyuma katika utoaji wa Elimu ya Juu hapa nchini.

Dkt. Kawambwa alisema hayo jana mjini Dodoma wakati akiongeza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Elimu kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane yaliyokuwa yanafanyika kitaifa mjini Dodoma.

Alisema katika Mpango huo Serikali inalenga kuboresha miundombinu ya ufundishaji na ujenzi wa hosteli nyingi kwa ajili ya kutatua tatizo la malazi kwa ajili ya wanachuo.

Dkt. Kawambwa alisema kuwa hatua hiyo pia inalenga kuwaendeleza wahadhiri kuanzia kwa ajili ya kusomesha katika Shahada za uzamili na uzamifu ili kupunguza tatizo la upungufu wa wahadhiri katika taalamu mbalimbali ambao watasaidia kuwaandaa vijana kuwa wataalamu katika fani mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa nchi.

Alisema kuwa ili kufanikisha zoezi hilo ya Chuo Kikuu kimoja hapa nchini kinaweza kuchaguliwa kuwa Kituo maalum cha kuwaanda na kuwafundisha wahadhari kutoka vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini.

Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kujenga msingi wa kuwa na viwango vya Elimu sawa kwa wahadhiri wa vyuo vikuu vyote hapa nchini katika sekta ya ufundishaji na hivyo kuwa na wataalamu waliopikwa vizuri.

Dkt. Kawambwa alisema kuwa baada ya kukamilka kwa maandalizi ya mpango huo vyuo vikuu 38 vinavyotoa elimu ya Juu hapa nchini vitakuwa na fursa ya kuelimisha walimu wao katika Chuo Kikuu ambacho kitakuwa kimechaguliwa kwa ajili ya kufundushia wahadhari.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...