Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, January 21, 2013

COSMOS GROUP YAZINDUA JENGO JIPYA LA UHURU HEIGHTS NAKUTOA FURSA KWA WATANZANIA KUNUNUA NYUMBA KWA MIKOPO KUPITIA BENKI
Muonekano wa Jengo la Uhuru Heights lililopo barabara ya Bibi Titi Mohammed liking'arisha jiji la Dar nyakati za usiku.Picha na Mo Blog

MC katika uzinduzi wa Jengo la Uhuru Hegihts Taji Liundi.

Mgeni rasmi Balozi wa Pakistan nchini Tanzania Tajammul Altaf akipokea shada la maua kutoka kwa watoto Ilsa na Alaisa ikiwa shukrani kwa kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa jengo la Uhuru Heights. Kushoto ni Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru Heights Muhammad Owasi Pardesi na wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa International Commercial Bank (Tanzania) LTD Basser Mohamed.

Ilsa na Alaisa wakiimba wimbo wa Taifa kubariki sherehe za ufunguzi wa jengo hilo.

Mgeni rasmi Balozi wa Pakistan nchini Tanzania Tajammul Altaf akizungumza katika uzinduzi huo ambapo amasema amefurahishwa na jitihada zilizofanywa na mfanyabiashara kutoka nchini kwake na jinsi Tanzania ilivyoweza kumpa ushirikiano na hatimaye sasa matunda yameonekana kwa kuzaliwa jengo la Uhuru Heights lenye hadi ya Kimataifa.
Aidha amesema huo ni mwanzo tu na kuwataka wafanyabiashara zaidi kutoka Pakistan kuja kuwekeza Tanzania kwa sababu mahali ambapo ukiwekeza matunda yanaonekana kutokana na amani na utulivu uliopo na ushirikiano wa serikali.

Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru Heights Muhammad Owasi Pardesi akizungumza na wageni wakati wa uzinduzi wa jengo hilo na kutoa shukrani zake akisema sasa wakazi wa Dar es Salaam wataweza kununua nyumba kwa njia ya mkopo kutoka Benki ya International Commercial (ICB) na kulipa kwa muda wa miaka 10 na kuishi katika miongoni mwa majengo marefu ya makazi yaliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam lililojengwa kwa gharama ya Dola za Kimarekani Bilioni 40.
Amesema Malengo ya kampuni ya Cosmos Group ni kuboresha miundo mbinu na maisha ya watu na hayo yamezingatiwa kwa kujenga jengo la Uhuru Heights.

CEO wa VFX Dubai Yusuf Thakur akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa International Commercial Bank (Tanzania) LTD Basser Mohamed akielezea wageni waalikwa jinsi watakavyoweza kufaidika na mikopo itakayotolewa na Benki hiyo ikiwemo kupata kipindi cha marejesho ya mkopo kwa miezi 120, viwango nafuu vya riba, kiwango cha juu cha umri wa mkopaji ni miaka 60 kufikia kipindi mkopo unapotolewa na mkopo huo unapatikana kwa hela za madafu na dola za Marekani.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya EXIM Anthony Grant akifafanua namna wateja wa Benki ya Exim watakavyoweza kunufaika na mkopo kwa ajili ya kununua nyumba zilizopo katika jengo la Uhuru Heights.

Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru Heights Muhammad Owasi Pardesi akipeana mikono na Afisa Mtendaji Mkuu wa International Commercial Bank (Tanzania) LTD Basser Mohamed (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya EXIM Anthony Grant (kushoto) ikiwa ni ishara ya kuingia mkataba wa kufanya biashara pamoja baina ya Cosmos, IBC Benki na Exim.

CEO wa VFX Dubai Yusuf Thakur akiendesha zoezi la mauzo ya nyumba katika jengo la Uhuru Heights ambapo mteja wa kwanza Samantar Abdinur Iusuf (kulia) aliyejitokeza kununua makazi katika jengo hilo.

Mgeni rasmi Mh. Tajammul Altaf akimpongeza mteja wa kwanz baada ya kununua moja ya nyumba kuashiria uzinduzi wa idara ya mauzo na wageni wengine pia kuendelea na manunuzi wakati wa uzinduzi huo.

Balozi wa Japan nchini Tanzania Salome Sijaona ( wa pili kushoto) akizungumza jambo la msingi wakati wakitembelea maeneo mbalimbali ya jengo hilo na Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru Heights Muhammad Owasi Pardesi. Kushoto ni mgeni rasmi Balozi Tajammul Altaf.

Wasanii wa kikundi cha ngoma za asili cha Safi Theatre wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la kisasa la biashara na makazi la Uhuru Heights jijini Dar.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...