Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, January 19, 2013

Ray, Wolpe wamteta Wema Sepetu kwa saa kadhaa


Jaqueline Wolpe ndio huyu
Na Mdakuzi Spesho, Dar es Salaam
WASANII wawili maarufu hapa nchini, Vicent Kigosi (Ray) na mwenzake Jaqueline Wolpe, siku nzima ya jana, waliitumia katika Viwanja vya Leaders Club, huku mazungumzo yao yote yakielekea kwa mrembwende wa zamani na mkali wa filamu Tanzania, Wema Abraham Sepetu.
Wema Sepetu akionyesha pozi lake
Hata hivyo mazungumzo hayo, hayakuwa mabaya sana kwa wasanii hao zaidi ya kuwaza namna gani ya kulinda majina yao yasishuke katika kipindi cha mwaka 2013 na 2014, huku mzungumzaji mkubwa akiwa ni Ray.
Vicent Kigosi, Ray
Wakati wa mazungumzo hayo, Wolpe alionekana kama mwenye shauku ya kutaka kufanyia kazi ushauri wa Ray, hasa kwa kuangalia zaidi nyota ya Wema Sepetu inavyozidi kung’aa, huku kila mmoja akitamani kumtaja au kumshika mkono.
Licha ya mazungumzo yao kuwa siri na wakiongea kwa sauti ya chini, lakini kipaza sauti cha mdakuzi wetu kiliwanasa na kusikia baadhi ya mambo waliyozungumza, ikiwamo ushindani wa sanaa, hasa kwa wasichana, akiwamo Wema, Wolpe, Aunt Ezekiel na Irene Uwoya.
Kwa mwaka Wema aling’ara sana, lakini wewe pia ulifanya kazi nzuri katika sanaa, hivyo nadhani kuna haja ya kuongeza kasi zaidi kwa ajili ya kufika malengo,” alisema Ray, akimwambia Wolpe aliyetega masikio yake kwa umakini.
Leaders Club hutumiwa watu mbalimbali kujipumzisha nyakati za mchana kutokana na kuwa sehemu tulivu, jambo linalowafanya wasanii na wengineo kukutana hapo wakibadilishana mawazo.
Makali ya Wema Sepetu yamezidi kutishia uwepo wa wasanii wa filamu wa kike hapa nchini, kutokana na kupendwa na watu wengi, jambo linaloongeza joto na msisimko kwa wanaofuatilia sanaa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...