Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, January 26, 2013

WATEJA WA VODACOM CHANGAMKIENI SHILINGI MILIONI 438 KUPITIA PROMOSHENI YA"MEGA SMS"


 Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Rukia Mtingwa
----
 Jumla ya Shilingi milioni 438 kushindaniwa kwa siku tisini(90).
Wateja wa Vodacom Tanzania mnakumbushwa kushiriki katika Promosheni kabambe ya"Mega SMS Promo" ambayo itamuwezesha mteja kujishindia hadi shilingi milioni moja papo hapo kila siku.
Aidha, mbali ya kujishindia kiasi hicho cha fedha kupitia kampeni hiyo kubwa na ya aina yake,pia kampeni ya Mega Promo  inatoa fursa kwa wateja wawili kujishindia hadi shilingi milioni 5 kila mmoja katika kipindi cha siku saba.

Jumla ya shilingi milioni 438 zinaendelea kushindaniwa ndani ya siku 90 nchi nzima,na wateja wote watakaoibuka washindi watajulishwa kwa njia ya simu sambamba na kupewa utaratibu maalumu wa kuchukua fedha zao zitakazotolewa kwa njia ya M-Pesa.

Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Rukia Mtingwa, amesema ili mteja aweze kuingia kwenye nafasi ya kushinda fedha hizo atalazimika kutuma ujumbe wa neno 'Mahela' kwenda 15544.

"Ili kujiweka katika nafasi kubwa ya kushinda unapaswa kutuma neno mahela kwenda 15544, baadaye utaulizwa maswali tofauti tofauti kupitia ujumbe mfupi na ukifanikiwa kujibu utajinyakulia shilingi milioni moja," anasema Mtingwa.

Anafafanua kuwa kupitia kampeni hiyo wateja watatu watakaoshinda kwa kujibu maswali vizuri waliyoulizwa kupitia SMS watajinyakulia  shilingi milioni moja kila mmoja kila siku. Wakati wengine wawili watakaojibu vizuri zaidi watajipatia hadi shilingi milioni 5 kila mmoja ndani ya siku saba.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...