Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, January 21, 2013

Mambo yameiva Kilimanjaro Marathon 2013



Waandaaji wa Kilimanjaro Marathon 2013 wametangaza kwamba maandalizi kwa ajili ya mashindano ya mwaka huu yanaendelea vizuri na mbio za mwaka huu zinatarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake. Mbio hizo zimepangwa kufanyika tarehe 3 Machi 2013 mjini Moshi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wild Frontiers, John Addison waandaaji wa tukio hilo alisema kwamba usajili wa washiriki utafanyika mjini Arusha tarehe 28 Februari katika hotel ya New Arusha, na tarehe 1 na 2 Machi usajili utafanyika Hoteli ya  Keys Moshi. Hakuna mtu ataruhusiwa kujisajili siku ya mashindano.

Usajili wa mtandao tayari upo wazi na washiriki wanaweza kuanza kujiandikisha kwenye mtandao kupitia tovuti ya www.kilimanjaromarathon.com.

Alisema, Kilimanjaro Premium Lager Marathon ya km 42, Nusu Marathoni ya km 21, na GAPCO Nusu Marathoni kwa walemavu zitaanzia uwanja wa MUCCoBs, wakati Vodacom  Fun Run ya km 5 itaanzia mashariki mwa geti la uwanja wa MUCCoBs kwa upande wa barabara ya Uru na kumalizika ndani ya uwanja.

Kilimanjaro Premium lager Marathon ya km 42 itaanza saa 12:30 asubuhi, na kufuatiwa na Km 21 Nusu Marathon kwa walemavu saa 12:45 Asubuhi na Km 21 Nusu Marathon itaanza saa 01:00 asubuhi wakati Vodacom Fun Run ya Km 5 inategemea kuanza 01:30 Asubuhi.“Kilimanjaro Marathon 2013 itapata usimamizi wa wataalamu wa riadha pamoja na wataalamu wa masuala ya muda (time-keeping) navilevile kutakuwepo vituo mbalimbali vya kunywa maji na viburudisho.

Addison aliongeza kuwa Kilimanjaro Marathon ni tukio ambalo limeendelea kuongeza  hadhi ya Tanzania kimataifa kila mwaka; na imesaidia kutambua na kutoa fursa kwa wanariadha wa ndani kukua zaidi, kukuza utalii wa Tanzania na watu kupata nafasi ya kufurahi zaidi.

Alisema mbio hizo zitakuwa na viwango vya kimataifa na kusimamiwa na Kilimanjaro Marathon Club, Athletics Tanzania na Kilimanjaro Amateur Athletics Association. Ili kuhakikisha usalama wa wakimbiaji, baadhi ya barabara za ndani na nje ya mji wa Moshi zitafungwa kuanzia saa 12:15 asubuhi hadi 03:30 asubuhi tarehe 3, Machi 2013 ili kuruhusu wakimbiaji kupita salama.

Tanzania Breweries Limited na bidhaa yao ya Kilimanjaro Premium Lager ni wadhamini wakuu wa Kilimanjaro Marathon na shughuli zingine za burudani baada ya riadha, na wamekuwa wadhamini wa tukio hili tangu kuanzishwa kwake mwaka 2003, juhudi zao katika masoko na matangazo imekuwa mchango mkubwa katika kukuza mbio hizi.

Executive Solutions ni waratibu wa tukio hilo wakati wadhamini wengine ni Vodacom Tanzania (Km 5 Fun Run), GAPCO (Nusu Marathon kwa Walemavu), Tanga Cement, CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, Tanzanite One, New Arusha Hotel, na Kilimanjaro Water.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...