Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, January 21, 2013

YANGA YAJINASIBU KUIFUNGA TENA BLACK LEOPARDS JIJINI MWANZA


Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Ernest Brandts amesema timu yake itafanya vizuri katika mechi ya marudiano ya kirafiki dhidi ya Black Leopards ya Afrika Kusini niliyopangwa kufanyika jumatano mjini Mwanza.
Brandts alisema wachezaji wake wote wamefikia kiwango kile anachotaka na mchezo huo utakuwa muhimu sana kwake kwani ni wa mwisho kabla ya kuingia katika kampeni za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Alisema kuwa Black Leopards ni timu nzuri na walipata mazoezi mazuri katika mechi ya kwanza iliyofanyika kwenye uwanja waTaifa jijini na kushinda kwa mabao 3-2.
“Ni mechi nzuri ambayo nadhani itakuwa ni kipimo kikubwa kabla ya kuanza kwa LigiKuu ya Tanzania Bara, wachezaji wangu wana viwango vizuri sana kwa sasa na naamini makosa yaliyofanyika katika mechi ya kwanza hawatayafanya tena,” alisema Brandts.
Kuhusiana na mabacha wawili, Mbuyu Twite na Kabanga Twite kucheza upande wa kulia, Brandts alisema kuwa wachezaji hao wana uwezo wa kucheza nafasi nyingi katika timu yake na uamuzi huo ulikuwa na faida kwa Yanga.
“Kabanga anauwezo wa kucheza nafasi ya ushambuliaji, katikati, beki zote na hata Mbuyu ana uwezo huo, hivyo uwepo wao katika timu ni mkubwa, niliwapumzisha kutokana na mipango ya mechi na wala si vinginevyo,” alisema.
Msemaji wa Klabu Yanga, Baraka Kizuguto alisema jana kuwa pamoja na mechi hiyo kuwa ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, pia wameamua kuicheza ili kuwapa burudani mashabiki wa Mwanza.
Kizuguto alisema kuwa Yanga haitakuwa na mechi yoyote katika mzunguko wa pili Kanda ya ziwa na hiyo ndiyo nafasi yao ya kuwapa waonyesha uwezo wao mkubwa mashabiki wa Mwanza nini wamekipata kutoka Uturuki.
“Tuna mashabiki wengi sana Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla, hii ni fursa kwetu kwani mahsbaiki na wanachama watapata fursa ya kuona kiwango na maandalizi ya timu yao kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili,” alisema Kizuguto.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...