Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, January 19, 2013

YANGA YAONYESHA VITU VYA UTURUKI MASHABIKI WAO LEO , YAITUNGUA BLACK LEOPARD 3-2Mshambuliaji wa timu ya Black Leopards FC ya Afrika Kusini, Joshua Obaje (kushoto) akijiandaa kupiga mpira mbele ya mlinzi wa timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam-Tanzania, Oscar Joshua wakati wa mchezo wa kirafiki baina ya timu hizo mbili uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Yanga imeshinda 3-2.
Heka heka langoni mwa Yanga... Mlinda Mlango wa Yanga, Said Mohamed akijaribu kuokoa hatari hiyo langoni kwake.
Wana Yanga kutoka Pugu Kigogo Fresh wao walikodi daladala kwenda kuona mchezo huo.
Mashabiki wa Yanga wakifuatilia game hilo l;a watoto wa 'Uturuki'
Frank Domayo wa Yanga (chini) akimshika shati Mlinzi wa Black Leopards, Humahrey Khoza.
Haooo wenyewe wakiimba
Weeeeeeee pisha nipite nimetoka Uturuki juzi ujue...
Hawa nao walikuwepo.
Baadhi naona hawajafurahia kiwango
Mlinzi wa Black Leopards, Humahrey Khoza akigangwa gangwa huku mlinda mlango wake Ayanda Mishal akimwangalia.
Abbas Amidu wa Black Leopards (kushoto) akiwania mpira na Oscar Joshua wa Yanga.
Watoa Huduma ya kwanza wakifuatilia game hilo
Walinda usalama walikuwepo wa kutosha
Hawa jamaa baada ya game kumalizika na wenzao wa Yanga kutimkia katika chumba cha kubadilishia nguo na mapumziko wao waliingia uwanhani na kunyoosha viungo kwanza ili misuli irudi katika hali yake ya kawaida.
Hiki ndiyo kikosi kazi cha Yanga
Kikosi cha Black Leopards ya Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...