Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, January 30, 2013

JACK PATRICK NUSU AMTOE ROHO MTU Mrembo aliyenusulika kuuwa na kipigo cha chupa kutoka kwa Jack Patrick, akiwa katika pozi muda mfupi baada ya kushonwa nyuzi tatu.
STAA wa Bongo anayetesa kwenye mitindo, Jacqueline Patrick anakabiliwa na msala wa kumtwanga na chupa nusu kumuua mrembo anayejulikana kwa jina la Hafsa Sasya, Risasi Mchanganyiko linanashuka nayo.
Habari zilizopenyezwa na chanzo chetu kutoka eneo la tukio zinasema kwamba, ishu ilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi ya Januari 26, mwaka huu ndani ya Ukumbi  wa Elements Lounge uliopo Masaki, Dar.
CHANZO KINATIRIRIKA
Huku sharti la kutotajwa jina lake gazetini likisisitizwa na chanzo hicho, kilisema: “Unajua yule dada (Hafsa) anasoma Kurasini na anaishi Kijitonyama, namfahamu vizuri sana. Walipokutana na Jack pale ukumbini palitokea kutokuelewana kidogo.

“Baada ya muda hali ikawa sawa, watu wakajua yamekwisa. Jack akaenda zake chooni, aliporudi alikuwa na chupa na kwenda kumpiga nayo Hafsa. Mabaunsa wakamwondoa Jack ukumbini na kumwingiza Hafsa kwenye gari lake kwa lengo la kumpeleka hospitalini. Kilichoendelea hapo sijui.”
PEKUPEKU ZA RISASI
Mwandishi wetu aliingia mzigoni rasmi na kuanza kuichimba kwa kina habari hiyo ambapo alipata uhakika wa kutokea kwa tukio hilo na Jack kufikishwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay ambapo alifunguliwa kesi yenye jalada namba  OB/RB/1678/13  KUJERUHI.
Baada ya kujiridhisha kwa hilo, zoezi lililofuata lilikuwa ni kuwatafuta wawili hao ili waeleze wanachokijua kuhusu tukio hilo. Wa kwanza kupatikana alikuwa ni Jack.
BOFYA HAPA KUMSIKILIZA JACK
“Ni kweli kulitokea ugomvi siku ile...na ni kweli nilihojiwa na Polisi wa Kituo cha Oysterbay, lakini nimetoka kwa dhamana na kesi imekwenda mahakamani.”
HUYU HAPA HAFSA
“Mimi na Jack tulikuwa marafiki lakini nashangaa amenipiga na chupa bila sababu. Nimeshonwa nyuzi tatu. Siku ile alinikuta nimesimama na rafiki yangu mara akanipiga kikumbo kisha akaenda chooni, aliporudi akanikumba tena, nilipomuuliza ikawa kosa; akanipiga na chupa.

“Imeniuma sana maana amenipa jeraha usoni mwangu bila sababu ya msingi, maana sina ugomvi naye. Kwa sababu hili suala lipo mikononi mwa sheria, naamini itachukua mkondo wake.”

Mrembo anayekwenda kwa jina la Hafsa akiwa katika hali mbaya muda mfupi baada ya kushushiwa kipigo kikali na Jack Patrick

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...