Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, January 19, 2013

MAWAZIRI WABAINI UFISADI MKUBWA BANDARINI


Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akimkaribisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdalah Kigoda walipofanya ziara ya kawaida ya mawaziri wanne ya kutembelea Mamlaka ya Bandari, Dar es Salaam leo. Wa tatu kushoto ni Waziri wa Fedha, Dk. William Mngimwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande aliye kushoto kwa Dk. Mwakyembe. (Picha habari na www.mwaibale.blogspot.com)
Na Dotto Mwaibale

MAWAZIRI wa nne jana walibaini ufisadi mkubwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA), kwa kuondolewa kipengele,  kinacho muelekeza  mkandarasi aliyejenga mtambo wa mafuta kutoa vifaa vyenye thamani ya sh bilioni 3 kwa ajili ya kuendesha mtambo huo.

Ufisadi huo ulibainika wakati  Mkurugenzi Mkuu wa PTA, Madeni Kipande alipotoa taarifa mbele ya mawaziri hao kuwa wamesikitishwa na kitendo cha kuondolewa kipengele hicho kilichofikiwa kati ya mamlaka hiyo na Kampuni ya ujenzi ya  Leinton ya Singapore.

"Iwapo mtambo huo uliofungwa ukiharibika itakuwa ni matatizo makubwa kutokana na sipea hizo tulizoahidiana kuto kuwepo kwani italazimaka kazi kusimama katika bandari yetu" alisema Kipande.


Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo ya Bandari Dar es Salaam jana katika ziara aliyoiita ya kawaida kutembelea Bandari hiyo ambayo ni kitega uchumi wa Taifa.

Mwakyembe pamoja na wenzake waliagiza haraka kupata maelezo ya watu hao  waliohusika kuondoa kipengele hicho kwenye huo mkataba na kusisita kuwa hiyo ni hujuma kwa Taifa.

“Ni jambo la cha kushangaza na kusikitisha kuona mkataba uliokwisha kamilika kwa kusainiwa unavunjwa kiaina, kwa jambo hili hatutaki mzaha tunaomba hadi Jumatatu mtupe majibu ili tuyafanyie kazi kwa pamoja”alisema Mwakyembe.



Mwakyembe aliitaka Bodi itishe kikao cha dharura ili hadi kesho lipatikane jibu kwa anaamini watu hao wanajulikana na wapo wala hawakp mbali.


 Mwakyembe alisema kama kutabainika kuwepo kwa mwanasheria yeyote aliyehusika katika kuuchezea mkataba huo kwa kuchomoa baadhi ya karatasi ajue nayeye atachomolewa bila huruma.


Mawaziri hao wakizungumzia kuhusu mashine ya utambuzi wa mizigo kwenye makontena (scan), ambayo inasimamiwa na TRA, Mwakyembe alisema hawaelewi ni sababu gani iliyofanywa  kupelekwa mkoani Tanga ambako ni zaidi ya miaka miwili sasa haifanyi kazi.

“ Jambo hili nalo linatushangaza kama mashine hiyo haifanyi kazi  imepelekwa huko kufanya nini au inacheza taarab”alihoji Dk. Mwakyembe

Mwakyembe aliigazi mamlaka hiyo kuhakikisha mashine hiyo inarudishwa ili ziweze kuwa mbili katika kuimarisha utendaji kazi katika bandari ya Dar es Salaam.

Alitaka Mamlaka hiyo kuhakikisha wanaanzisha mtandao utakaoviwezesha vitengo vyake vyote e kufanya kazi kwa wakati mmoja ili kupunguza urasimu na mianya ya rushwa katika bandari hiyo.

Mawaziri waliokuwepo katika ziara hiyo mbali ya  Dk. Mwakyembe ni  Waziri wa Fedha wa Fedha wa Fedha Dk. William Mgimwa, Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah Kigoda, na Naibu Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...