Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, January 28, 2013

DHAMANA YA LULU MAHAKAMANI LEO, MASHART LAINIIIII KAMA UNANAWA! Kula bata uraiani


Msanii wa Filamu nchini Elizabeth Michael (Lulu) akizungumza na wakili wake Peter Kibatala muda mfupi kabla ya kuanza kusikilizwa ombi lake la dhamana leo asubuhi kwenye Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam ambapo dhamana hiyo imepatikana kwa mashart ya mashahidi wawili wafanyakazi wa Serikali kwa bondio ya fedha Tsh20 Millioni kila mmoja na masharti mengine tumeorodhesha kwenye habari hapo chini.
Msanii Lulu (katikati) akisubiri kusikiliza maombiyake ya dhamana kusomwa na Jaji anaesikiliza kesi hiyo Zainabu Mruke leo jijini Dar es Salaam.
Lulu akiwasili kwenye kizimba cha Mahakama kuu jijini Dar es Salaam leo.
Kama ilivyo sikuzote ulinzi uliimarishwa kwenye mahakama hiyo wakiwemo askari wakiume pamoja na wakike kumlinda msanii huyo.
Baada ya kusomewa mashart ya dhamana Lulu akiondoka huku akitokwa na machozi yanayoashiria furaha.
Ndugu jamaa na marafiki wa msanii huyo na baadhi ya watu wengine wakiwa kwenye Chumba cha mahakama kuu jijini Dar es Salaam wakisubiri kusikiliza maombi ya dhamana.
Msanii Muhusin Awadi (Dk.Cheni) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutolewa kwa dhamana ya msanii huyo.
Wakili wa Lulu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mteja wake kupatiwa dhamana.
 HATIMAYE Msanii wa Filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu mchana wa leo amepata dhamana na kuachiliwa kutokana na kesi inayo mkabili ya kuua bila kukusudia msanii mwenzake wa filamu marehemu Steven Kanumba  mwaka jana.
Akisoma mashart ya dhamana Jaji anaesikiliza Kesi hiyo Zainabu Mruke, alitaja mashart kadhaa ambayo mtuhumiwa atatakiwa kuyatekeleza kabla ya kupewa dhamana hiyo. 
Mruke alisema mtuhumiwa atatakiwa kuwasilisha hatizake za kusafiria zote mahakamani hapo, atatakiwa kuwa na wadhamini wawili wafanyakazi wa serikali ambao kila mmoja atatakiwa kuweka udhamini wa Tsh20Millioni kama bondi na sio keshi.
Aidha Jaji Mruke aliongeza kuwa mtuhumiwa hataruhusiwa kusafiri nnje ya jiji la Dar es Salaam isipokuwa kwa ruhusa maalum ya mahakama, lakini pia atatakiwa kuripoti mahakamani kilatarehe moja ya kila mwezi.
Wakili wa mshtakiwa huyo Peter Kibatala alisema amefurahishwa na dhamana aliyopatiwa mtejawake na wataendelea na kazi ya kumtetea hadi mwisho wa kesi hiyo.
Wasanii wenzake waliojitokeza na kuonekana mahakamani hapo ni pamoja na Muhusin Awadh (Dk.Cheni) na Steve Nyerere. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hukumu hiyo Dk.Cheni alisema yeye binafsi amefurahishwa na dhamana hiyo na yuko tayari kufanyanae kazi.
“Lulu nilimchukua kwao akiwa na miaka mine na kuanza kufanyanae kazi hadi sasa akiwa na umri wa miaka 18 amekua msanii mkubwa nan i Director mzuri pia kwahiyo nitaendelea kufanyanae kazi”Alisema Dk.Cheni.
Alipoulizwa kuhusu kutimiza Mashart ya dhamana Dk.Cheni alisema kila kitu kilikuwa kimetimia ispokuwa passport tu ndio hawakutarajia kama ingehitajika lakini tayari alishapigiwa simu mtu ailete kutoka nyumbani kwao Tabata na kukamilisha mashart ya dhamana hiyo. 

April saba mwakajana msanii huyo alifikwa na kadhia hiyo ya tuhuma za kumuua bila kukusudia msanii mwenzake wa Filamu nchini marehemu Steven Kanumba kutokana na mgogoro uliotokana na wivu wa kimapenzi, baada ya kuelezwa kuwa wawili hao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi. 
 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...