Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, January 26, 2013

MAULID YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W)YAFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA MAISARA


IM 6380Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, alipowasili katika viwanja vya Maisara katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana, na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Amani Abeid Karume,(katikati).
IMG_6367Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maulid EL Nabii Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis,alipowasili katika viwanja vya Maisara katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana.
IM   6404Ustadh Rashid Jaffer wa Magogoni Mjini Zanzibar,akisoma Quran Tukufu ya Ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya Kiislamu.
IM   6412Ustadh Abdulla Hamad wa Chuo cha Kiislamu,akitoa tafsiri ya Aya za Quran,zilizosomwa na Ustadh Rashid Jaffer wa Magogoni Mjini Zanzibar,akisoma Quran Tukufu ya Ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja
vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya Kiislamu.
IM 6374Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Viongozi wa Jumuiya ya Maulid EL Nabii Zanzibar,alipowasili katika viwanja vya Maisara katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...