Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, January 24, 2013

MISS UTALII VIPAJI KUFANYIKA JUMAPILI IKONDOLELO




Tamasha kubwa la vipaji litafanyika katika Ukumbi wa Ikondolelo Lodge Hoteli ya Kitalii Kibamba Jumapili hii, Januari 27, 2013, ambapo warembo zaidi ya Thelasini wataingia katika kuonesha vipaji mbalimbali vikiwemo na, Kucheza ngoma, Kuimba, pamoja kuonesha mavazi mbalimbali ya Asilia.

Katika Tamasha hilo Maalum Mgeni Rasmi atakuwa Muheshimiwa Iddy Azan Zungu Mbunge wa Jimbo la kinondoni.

Sambamba na Hayo Muheshimiwa Zungu atazindua tuzo Mbalimbali za Utalii Tanzania, kama Tuzo ya Mazingira, Tuzo ya Utamaduni, Tuzo ya Jinsia, wanawake na watoto, Tuzo ya Polisi Jamii, Tuzo ya Elimu ya Jamii, Tuzo ya Hifadhi ya Serengeti, Tuzo ya Mlima Kilimanjaro, Tuzo ya Michezo pamoja na Tuzo zengine mbalimbali.

Viingilio katika Tamasha hilo vitakuwa kama ifuatavyo, V.I.P 20,000 , Watu wa kawaida 10,000 na watoto 5,000
Tamasha litaanza kuanzia sa nane mchana na kuendelea

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...