Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, January 20, 2013

MCHEZO WA SIMBA NA TIMU YA JESHI LA OMANMabingwa wa soka Tanzania bara, Simba jana walipoteza mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Timu ya Taifa ya Jeshi la Oman kwa magoli 3-1 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Qaboos complex jijini Muscat.Bao pekee la kufutia machozi la Simba liliwekwa kiamiani na mshambulaiji wake Haruna Moshi 'boban' katika kipindi cha pili.


Mwenyekiti wake Ismail Aden Rage alikuwa jukwaani pamoja na viongozi wengine wa simba, mdhamini wa safari hiyo Rahma Al Kharusi na Musleh Rawahi pamoja na kocha Talib Hilal wakiishuhudia simba ikizama mbele ya wanajeshi hao ambao kikosi chao kina wachezaji tisa wanaocheza timu ya taifa ya oman.

Picha kwa Hisani ya Saleh Ally wa Champion-GPL.
Simba walipofunga goli.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...