Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, January 28, 2013

MASHAIRI YAMUUMIZA KICHWA PINGUNa Elizabeth John
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ramadhani Kalesela ‘Pingu’ amesema kuwa anafanya uchaguzi wa nyimbo alizonazo ili kuachia mojawapo ambayo itakonga na kuteka soko la muziki nchini.

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Pingu alisema anapata wakati mgumu kuchagua wimbo wa kuachia kutokana na kila wimbo kuwa katika kiwango cha juu.

“Nyimbo zangu zote ni nzuri kitu ambacho kinanipa wakati mgumu kuamua ni ngoma gani niachie lakini wakati wowote kuanzia sasa nitaachia baada ya kushauriana na wadau wangu,” alisema Pingu.

Msanii huyo alipata umaarufu kupitia nyimbo mbalimbali akishirikiana na Deso ambao walitoa albamu kadhaa ikiwemo inayoitwa ‘Eeh Mola’ iliyokuwa na nyimbo kama Tutasema, Hamisi, Chanzo Cha Ukoloni, Joanitha na nyinginezo.

Pia siku chache zilizopita msanii huyo aliachia ngoma yake ambayo haikufanya vizuri iliyoitwa ‘Zarumenda’ na sasa anajipanga upya kuhakikisha na anarudi tena katika tasnia hiyo akiwa pamoja na Deso.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...