Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, January 28, 2013

MKANDA WA NGUMI WA JUMUIYA YA MADOLA (CBC) WAGOMBEWA.JANUARY 28, 2013
 Mtanzania Fadhili Majia sasa atamvaa Mghana Isaac Quaye tarehe 8 March kutafuta nafasi ya kugombea mkanda wa ubingwa wa Jumuiya ya madola (CBC) ambayo unashikiliwa na bondia Kevin Satchell  wa Uingereza.

Mpambano wa Majia na Quaye umemsogezwa mbele kwa kuwa mashindano ya ubingwa wa Afrika yanayoendelea nchini Afrika ya Kusini yanarushwa na televisheni ya Super Sports ambayo ndio wafadhili wakubwa wa mpambano wao.

Wakati huo huo bondia Richard Commey wa Ghana atamvaa Mghana mwenzake Bilal Muhammed kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati uzito wa lightweight siku hiyo hiyo March 30. Aidha bondia Frederick Lawson wa Ghana atazichapa na bondia Isaac Sowah wa Ghana kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati  katika uzito wa Welterweight. Mapambano hayo yatasimamiwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Mtanzania Onesmo Ngowi

Mtanzania mwingine atakaye peperusha bendera ya taifa siku hiyo ni pamoja na Allan Kamote atakayezichapa na bingwa wa zamani wa IBF wa mabara na ambaye ndiye bingwa wa sasa wa WBA wa mabara Emmanuel Tagoe katika pambano lisilo la ubingwa.

Naye bondia wa Kenya Michael Odhiambo atachuana vikali na Mghana George Ashire katika mpambano usio wa ubingwa uzito wa lightweight.

Mapambano hayo yote yatakuwa ni ya utangulizi katika mpambano wa ubingwa wa dunia kati ya bondia maarufu wa Ghana anayeishi nchini Marekani Joseph Agbeko na Luis Mendelez kutoka nchini Columbia.

IBF/Afrika inawaomba watanzania kwa ujumla wao wawaombee mabondia wake ili waweze kupeperusha vyema bendera ya taifa.

Imetolewa na:
UTAWALA
International Boxing Federation Africa
DAR-ES-SALAAM

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...