Kampuni ya simu za mkoni Airtel Tanzania imempata mshindi wa milioni 50 na kuongeza muda wa promiosheni hiyo kwa kipindi chote cha mwezi wa ramadhan huku ikiwa imewazawadia wateja wake jumla ya shilingi milioni 305 hadi kufikia jana.
Katika kauli iliyotolewa na meneja uhusiano wa Airtel Jackson mmbando alisema” leo tunampatia mshindi mkuu wa promotion ya kwanjuka kwa kipengele cha kwanza na pia tunaongeza muda wa promosheni pamoja na zawadi.
Kuanzia sasa washindi watajishindia shilingi milioni moja kila siku na shilingi milioni 5 mwishoni mwa wiki wakati katika kilele mshindi kwenye droo kubwa ataondoka na shilini milioni 20 pesa taslim.
Promosheni ya kwanjuka imeongezewa muda wa siku 31 na itahusisha wateja wote wa Airtel Tanzania watakaoshiriki, Ili kushiriki mteja anatakiwa kutuma neno KWANJUAKA kwenda namba 15656 kisha mteja atapata maswali na akiyajibu kwa usahihi atajiongezea pointi za kuwa mshindi.
Leo hii Tumefikia kilele cha promosheni hii tangu ilipoanza Aprili 2011, lakini kutokana na faida nzuri tuliyopata pamoja na wateja wetu kuipenda sana promosheni hii basi tumeamua kuongeza zawadi pamoja na muda wa wateja kushiriki katika promosheni hii.
Leo mshindi wa milioni 50 wa droo kubwa sehemu ya kwanza ya promosheni hii ni Andew Isaya Goha Father wa kanisa katoliki Parokia ya Mofu Mahenge Mkoani Morogoro, umri wake miaka 48
Aidha meneja wa bidhaa na mawasiliano Rahma Mwapachu aliongeza kwa kusema, Airtel inawahimiza wateja kuendelea kushiriki katika shindano hilo, ambalo limeongezwa muda wake na linaendelea ili wateja kupata nafasi za kujishindia zawadi mbalimbali , tunafuraha kuwajulisha kuwa promotion hii imekuwa ya mafanikio na washindi wamepatikana kutoka sehemu mbalimbali nchini, huku ikiinua maisha yao ambayo ndiyo lengo halisi la promosheni hii.
Kampuni ya Airtel inawaahidi watanzania kuendelea kupanua mtandao weke zaidi ili uweze kuwafikia wananchi wote hasa wale waishio vijijini kote nchini, Mwezi uliopita Airtel ilizidua huduma zake kwenye zaidi ya miji na vijiji 50 ikiwa ni katika kutimiza lengo lake la kuwafikia watu wengi na kuinua kiwango cha maisha yao na nchi nzima kwa ujumla
No comments:
Post a Comment