Askari Polisi wakimdhibiti kijana aliyekuwa akishukiwa kuwa jambazi, ambaye alifanya fujo kwa kupiga mawe vioo vya benki ya CRDB,Posta Mpya, Dar es Salaam jana na kusababisha wateja na wananchi kukimbia ovyo.Picha Zote Kwa Hisani Ya Kassim Mbarouk
---
Na Richard MwaikendaTAFRANI imetokea katika Benki ya CRDB, tawi la Azikiwe,baada ya kijana mmoja aliyehisiwa kuwa jambazi kurusha mawe kwenye vioo vya benki hiyo na kusababisha wateja kukimbia ovyo wakidhani wamevamiwa.
---
Na Richard MwaikendaTAFRANI imetokea katika Benki ya CRDB, tawi la Azikiwe,baada ya kijana mmoja aliyehisiwa kuwa jambazi kurusha mawe kwenye vioo vya benki hiyo na kusababisha wateja kukimbia ovyo wakidhani wamevamiwa.
Tukio hilo lilitokea jana mchana, ambapo kijana huyo anayedhaniwa kuwa akili yake imeathirika kwa kubuia dawa la kulevya 'Teja' kurusha mawe kuelekeza kwenye jengo hilo na kuvunja vioo.Baadhi ya wateja walianza kutimua mbio kutoka nje huku wengine wakilala chini kuhofia maisha yao.Baada ya kuona hivyo, Polisi waliokuwa kwenye lindo la benki hiyo, walifyatua risasi juu wakidhani majambazi wamevamia benki hiyo.
Lakini baada ya muda walimuona kijana huyo aliyekuwa katikati a Barabara ya Azikiwe karibu na kituo cha Daladala cha Posta Mpya, akiendelea kurusha mawe.Polisi walimuendea na kufanikiwa kumdhibiti na kuanza kumpatia mkong'oto wa nguvu, huku wanachi wenye hasira wakitaka nao waruhusiwe kumwadhibu.Ndani ya benki hiyo hali ilikuwa shaghalabaghala, kwani mitungi ya maua na baadhi ya nyaraka zilitawanyika ovyo, huku wakioneakana baadhi ya wateja wakiwa wamezirai na wengine wakilia baada ya kupotelewa na nyaraka muhimu za benki vikiwemo kadi na fedha taslimu.
Wakati tukio hilo ilitokea, pia hali haikuwa nzuri kwa wafanyakazi wa benki hiyo, kwani baadhi walisikika kuwa walipatwa na hofu kubwa kiasi cha baadhi yao kukimbilia kujificha vyooni na kuacha kaunta zao.
No comments:
Post a Comment