Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, August 1, 2011

Precision Air kupokea ndege mpya aina ya Boeing 737-300 wiki hii

Precision Air kupokea ndege mpya aina ya Boeing 737-300 wiki hii

Mkurugenzi wa Biashara Precision Air Bw. Phil Mwakitawa akizungumza katika hafla fupi iliokutanisha shirika la ndege hiyo na wadau wake katika utangulizi wa kuzindua safari za Hahaya, Comoro na Johannesburg, Afrika Kusini. Hafla hiyo ilifanyika Southern Sun Hotel jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita. Mkurugenzi huyo alisema kwamba wako tayari kupokea ndege yao mpya aina ya Boeing 737-300 wiki hii kutoka Luton, London-Uingereza tayari kwa kuanza safari za Comoro tarehe 17 na Johannesburg tarehe 24 mwezi huu wa Agosti.
Kaimu Meneja wa Mawasiliano na Masoko wa Precision Air, Bi. Elizabeth Mungwe (Kulia) akiwa na Meneja Mauzo Bw. Prosper Lawrence na Afisa wa Mauzo Bi. Happiness Gachuma, wote kutoka The Citizen.
Meneja wa Kenya Airways nchini Tanzania Bi. Lucy Malu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Biashara wa Precision Air Bw. Phil Mwakitawa katika hafla fupi iliyofanyika Southern Sun Hotel katika utangulizi wa kuzindua safari za Hahaya-Comoro kwa dola 47 na J'burg-Afrika kusini kwa dola 57.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Allan Sharra (kulia) akizindua dansi baada ya kutoa hotuba yake ilyoongelea ufanisi wa ndege yao mpya aina ya Boeing 737-300 itakayofika wiki hii. Alisema ndege hiyo itaongeza idadi ya wasafiri kutoka 17,000 kwa wiki hadi kufikia 70,000 kwa wiki.
Mawakala mbali mbali wa usafirishaji wa anga pia walikuwepo katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Precision Air.
Wadau wa Precision Air wakitoa 'cheers' kwa ishara ya kuzindua safari za Hahaya na Johannesburg na kupokea ndege mpya ya Boeing 737-300

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...