Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, August 1, 2011

FIESTA..... 1O years of History was marked!


Usiku wa kuamkia jana ulikuwa gumzo ktk viwanja vya Lidaz Kinondoni ambapo lile tamasha kubwa Afrika ya mashariki 'FIESTA' lilihitimishwa kwa show kali kutoka kwa LUDACRIS........ watu wengi kupita maelezo walimiminika ndani na nje ya uwanja


Show zilianzishwa na wasanii mbalimbali kutumbuiza, wengine wakashangiliwa na wengine kuzomewa kwa Sauti kubwa ya umati, ktk walioshangiliwa na kuzomewa wapo wasanii wawili zaidi Bushoke na Izzo B ambao makelele waliyopigiwa yana maana kubwa sana na hayatakiwi kupuuzwa kabisa!

Bushoke alizomewa sana pale alipoanza kuifagilia serikali eti imefanya mambo mazuri mengi sana, umati mkubwa wa vijana ukapinga ktk staili hio

Izzo B ndie aliyeshangiliwa sana zaidi alipoimba kile kibao chake cha "RIZ ONE Ongea na Msure" nyimbo inayomwelekeza Riz aongee na mkubwa juu ya mambo ya serikali ambayo mengi hayajakaa sawa! pia alipotaka umati uzomee TANESCO, umati ulizomea saaaaana!

10 Years of Fiesta, si mchezo.........


sehemu ya umati uliofurika

Diamond alipiga bonge la Show

dancers wa Diamond

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...