Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, September 13, 2011

Azam FC yawazima Villa SquadAZAM FC, leo imerekebisha makosa yake, na kufanikiwa kuichapa Villa Squad mabao 2-0, katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam.

Jumapili, timu hiyo iliumana na Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, lakini washambuliaji walishindwa kutumia vizuri nafasi nyingi za wazi walizopata, mpaka wakatoka uwanjani wakiwa hawajafungana.

Dakika ya kwanza, Kipre Tcheche, aliwainua mashabiki wa Azam kwa kuifungia timu yake b

ao la kwanza kwa shuti kali lililotemwa na kipa wa Villa, Abbas Nasoro.

Bao hilo liliwafanya Azam FC wazidi kulisakama lango la wapinzani wao, ambapo dakika ya 35, John Bocco aliifungia timu yake bao la pili kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Tcheche.

Bocco katika mechi dhidi ya Simba, alipata nafasi tatu nzuri, lakini alishindwa kuzitumia vizuri, katika mchezo wa jana alirekebisha makosa yake na kufanikiwa kuifungia timu yake bao hilo.

Mchezo huo ambao ulitawaliwa na rafu nyingi, huku pande zote mbili zikishambuliana kwa zamu.

Villa Squad walikianza kipindi cha pili kwa kasi na kulisakama lango la wapinzani wao, lakini Mohamed Kijuso, alikosa bao baada ya shuti lake kudakwa na kipa Mwadin Ally dakika ya 82.

Haruna Shamte wa Villa Squad, alipata nafasi nzuri ya kufunga, lakini shuti lake kali lilitoka nje ya lango la Azam.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...