Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, September 18, 2011

QUEENS, TWIGA STARS KUWASILI LEO


WASHINDI wa pili katika michuano ya All Afrika Game (AAG) timu ya Taifa ya Netiboli ‘Taifa Queens’, pamoja na timu ya soka ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ zinatarajiwa kuwasili kesho kutoka Maputo, Msumbiji ilipokuwa ikifanyika michuano hiyo.
Katika michuano hiyo ambayo Netiboli pekee iliitoa kimasomaso Tanzania kwa nafasi hiyo na kutwaa medali ya Fedha, iliwakilishwa pia katika michezo ya Ngumi za Ridhaa, mashua riadha, judo na paralimpiki.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA),Rose Mkisi aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kuipokea timu hiyo ili kuwatia moyo wachezaji wake ambao walicheza kufa kupona na kushika nafasi hiyo.

Alisema wanafanya utaratibu ili kuweza kuipongeza timu hiyo kwa kuweza kufanya vema na kuongeza kuwa wachezaji watapewa mapimziko mafupi kabla ya kuingia kambini kujiandaa na michezo mingine ambayo itashiriki.

Qeens ilipata medali hiyo baada ya kuifunga Botswana magoli 43-35 katika mchezo uliopogwa juzi kwenye uwanja wa Munhuana Maputo, Msumbji, huku Uganda ilishika nafasi ya kwanza na Zambia ikishika nafasi ya tatu.

Aidha, Twiga Stars nayo iinatarajiwa kuwasili saa nane mchana kwa ndege ya shirika la LAM.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...