Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, September 18, 2011

KASEBA KUMVAA MTAMBO WA GONGO


BONDIA Japheth Kaseba anajiandaa kupanda ulingoni dhidi ya Maneno Osward pambano lisilo la ubingwa litakalochezwa Oktoba Mosi Mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana,mmoja wa mabondia hao, Kaseba alisema litachezwa kati ya ukumbi wa Travertine Magomeni au DDC Mlimani ambapo litasimamiwa na Shirikisho la Ngumi za kulipwa Tanzania (PST).

Alisema pambano hilo ni ra raundi 10 uzito wa kati kilogramu 72 ambapo ni mara ya kwanza kwa mabondia hao kutwangana.

"Tupo katika maandalizi na hili limeandaliwa na mdau mmoja wa ngumi anayefahamika kwa jina la Gervas Mganda kwa kushirikiana na PST (Shirikisho la Ngumi za kulipwa Tanzania).," alisema

Alisema "nipo katika mazoezi kama ilivyo kawaida katika kambi yangu, wadau tunawaomba wajiandae kushuhudia pambano hili, lengo kuendeleza rekodi zetu na kuwapa burudani mashabiki.," alisema Kaseba.

Mbali na pambano hilo Kaseba amewahi kupambana na bondia Ernest Bujiku, Fransis Cheka, na Mada Maugo ambapo ameshinda moja kati ya hayo dhidui ya Bujiku.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...