Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, September 12, 2011

FLOYD MAYWETHER KAPAMBANA NA VICTOR ORTIZ


LOS ANGELES, Marekani


FLOYD Mayweather Jnr le atapanda ulingoni Septemba 17,2011 kupambana na Victor Ortiz kuwania ubingwa wa WBC.


Mayweather Jnr amekuwa kama ng'ombe wa maziwa wa kutoa fedha katika ngumi, licha ya kuwa nchi yake imekwua na matatizo ya kifedha wahasibu wa nyota huyo hawana mashaka na jambo kama hilo.


Atapambana na Victor Ortiz kuwania ubingwa wa dunia wa WBC uzani wa welter mjini Las Vegas wiki ijayo.Pambano hilo litaoneshwa katika Primetime na Mayweather anatarajia kuaingia pauni milioni 25 kwa kupitia televisheni hiyo.


Katika mapambano yake yaliyopita ambayo watu walikuwa wakilipia ili kuona alikusanya jumla ya pauni milioni

250.


Licha ya kuwa ni bingwa wa dunia mara tano na hajapigwa katika mechi zake 41,

Mayweather amepigiwa kura chache za umaarufu.


Anatwangana na Ortiz ambaye alikimbiwa na mama yake wakati akiwa na umri wa miaka saba na baba yake alikuwa na kawaida ya kupinga hadi alipoondoka.Victor ambaye sasa ana umri wa miaka 24,alianza ngumi akiwa na miaka 10 kabla ya kaunza ngumi za kulipwa akiwa na miaka 17, aliwahi kufanya bishara ya kuuza dawa za kulevya.


Kocha Rolando Arellano alisema: "Victor ame[ita katika mageti mageti ya ahera. Ni mtu mbaya ulingoni."


Kikikaririwa na gazeti la Sun Ortiz alimwelezea mpinzani wake akisema: "Floyd ni mpiganaji mzuri lakini sikuwahi kufikia ri kuwa mzuri sana."


Inaonekana kuwa Mayweather anaweza kuwandabisha kwa maneno yake.


Baada ya pambano hilo pengine linaweza kuwepo pambano jingine linasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa ngumi kati ya

Mayweather na Manny Pacquiao,

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...