Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, September 18, 2011

MSECHU JUKWAA MOJA NA EVE, SHAGGY


PETER MSECHU
EVE
SHAGGY

WASHINDI wa shindano la Tusker All Stars 2011, Mtanzania Peter Msechu, Mganda Davis Ntare na Mnyarwanda Alpha Rwirangira, wanatarajiwa kutumbuiza katika tamasha maalumu na wasanii mbalimbali wa kimataifa akiwamo mwanadada mkali wa Hip Hop kutoka nchini Marekani, Eve Jihan Jeffers, maarufu kama Eve.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi, Msechu alisema tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Oktoba mosi katika viwanja vya Carnivore huko Nairobi nchini Kenya.
Alisema anajisikia faraja kupata nafasi ya kupanda jukwaa moja na wasanii kubwa na wenye uzoefu wa muda mrefu hivyo anaamini kupitia onyesho hilo ataendelea kupata funzo kubwa katika jitihada zake za kupiga hatua za kimuziki.
Wasanii wengine watakotumbuiza ni pamoja na Ivo Manuel Lemus a.k.a Cabo Snoop kutoka Angola, mkali wa Dancehall na Ragga, Orville Richard Burrell, maarufu kama Shaggy kutoka nchini Jamaica na wengineo.
Msechu na wenzake wamepata nafasi hiyo baada ya kushinda shindano la Tusker All Stars 2011 lililomalizika mwezi Agosti Nairobi, Kenya.
http://mamapipiro.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...