Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, September 11, 2011

Mfuasi Wa CCM Amwagiwa Tindikali Igunga


Katibu wa uchumi na Fedha Taifa, ambaye pia ni Mratibu wa Uchaguzi wa CCM, jimbo la Igunga, Mwigulu Nchemba, akimtazama Musa Tesha, mfuasi wa CCM, aliyemwagiwa tindikali na watu wasiojulikana jana usiku mjini hapa.
MFUASI wa CCM, Mussa Tesha (24) akiwa katika hospitali ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, leo. Tesha ameungua usoni na sehemu kadhaa mwilini baada ya kumwagiwa tindikali usiku wa kuamkia leo na watu wanaohisiwa kuwa ni wafausi wa CHADEMA, ambapo inaelezwa kuwa walimwagia tindikali hiyo alipokuwa katika harakati za kupandika mitaani mabango ya mgombea wa Ubunge jimbo lgunga kwa tiketi ya CCM. Tesha amehamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Sala majira ya saa saba mchana wa leo kwa ndege ya kukodiwa ambayo za kukodi ndege hiyo na tiba zote zinalipwa na CCM. Picha na Vioctor Makinda

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...