Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, September 18, 2011

DIAMOND, LADY JAYDEE, TID WATINGA KISIMA AWARDS


VIDEO za wasanii wa muziki wa bongo fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee. Khaleed Mohammed ‘TID’ na Nassib Abdul ‘Diamond’ zimetajwa kuwania tuzo za tisa za muziki nchini Kenya maarufu kama ‘Kisima Awards ’ kwa mwaka 2011.
Wasanii hao wametajwa kuwania kipengele hicho kati ya 10 vya tuzo hizo zinazotarajiwa kufanyika Septemba 30 mwaka huu, ambapo mshindi wa kila kipengele ataondoka na fedha taslimu shilingi mil. moja za Kenya (zaidi ya shilingi mil. 13 za Tanzania).Wakati Diamond ameingiza wimbo wake wa Mbagala chini ya mtayarishaji Adam Juma, TID & Top Band ameingia na video ya Aisha iliyotayarishwa pia na Adam Juma, huku Lady Jaydee atawakilisha na Nitafanya, alioimba na Kidumu, video ambayo imetayarishwa na Robert Kimanzi & R Kay.
Aidha, kipengele hicho pia kitawaniwa na video za Coming Home ya Sauti Sol ambayo imetayarishwa na Willie Ousu, Land lord ya Mejja, iliyotayarishwa na Charles Luche, pamoja na Haturudi Nyuma ya Julianna Kanyemozi & Kidum iliyotayarishwa na R Kay.


Pia singo ya Nitafanya iliyoombwa na Lady Jaydee & Kidum nayo imepenya katika kipengele cha wimbo bora wa ushirikiano, ambapo watachuana na Little things you do (Wahu Feat, Bobi Wine), She Said Dat (Wyre Ft Cecile), Nitafanya (Kidum Ft Lady Jaydee), I’m here (Kdenk & Sana), Papa God Oh (MOG & Mr Seed) na Kila Moja (Nonini, Chege & Lady bee).

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...