Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, September 18, 2011

KUNDI LA T-MOTO LASOGEZA MBELE UZINDUZI ILI KUOMBOLEZA MSIBA WA MELI YA SPICE


KUNDI jipya la Taarab linalokwenda kwa jina la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) limesogeza mbele uzinduzi wake uliokuwa ufanyike Septemba 30 mwaka huu hadi Oktoba 28.


Kundi hilo lililoondoka jijini na kuweka kambi ya maandalizi katika Visiwa vya Zanzibar hivi karibuni, limeamua kusimamisha mazoezi yake kwa muda wa wiki moja na nusu kufuatia msiba mkubwa ulioikumba nchi kutokana na ajali ya meli ya Spice iliyozama eneo la Nungwi hivi karibuni na kusababisha vifo vya watu wengi na majeruhi ikiwa ni idadi ambayo haijawahi kutokea katika Visiwa hivyo.

Akizungumza na mwadishi wa habari hizi, Mkurugenzi wa kundi hilo, Amini Salmini, ambaye ni mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Salmini Amour ‘Komandoo’, alisema kuwa kutokana na kundi hilo kutambua ukubwa wa msiba huo ulio na idadi kubwa ya vifo vya watu kulinganisha na idadi ndogo ya watu waishio visiwani humo, wameamua kusitisha kambi ya mazoezi yao ikiwa ni sehemu ya kundi hilo kuwa katika maombolezo.

Aidha amesema kuwa wasanii wa kundi hilo wataendelea kubaki kambini bila kuendelea na mazoezi hayo ya maandalizi ya uzinduzi wao, hadi baada ya wiki moja na nusu kuanzia siku ya kwanza kati ya tatu za maombolezo zilizotangazwa na Serikali ya Zanzibar.

Kundi hilo linatarajia kuwasili jijini wiki ijayo kwa ajili ya kuingia studio kurekodi nyimbo zake mbili zilizokwisha kamilika na kurejea tena Zanzibar kuendelea na kambi hiyo.

“Kwa vile tayari kundi langu lilikwishakamilisha baadhi ya nyimbo, litakuja jijini wiki ijayo kurekodi nyimbo mbili na baada ya kumalizo zoezi hilo watarejea Unguja kuendelea na kambi ili kukamilisha mengi kati ya mazuri tuliyojipanganayo kuwaonyesha mashabiki wa muziki wa Taarab siku hiyo ya uzinduzi, Oktoba 28,

Na pia tumeamua kusogeza uzinduzi wetu tarehe ya mbali zaidi ili kuweza kufanya maandalizi ya kutosha baada ya kusitisha mazoezi yetu kwa muda wa wiki moja na nusu kwani msiba huu ni wa kitaifa na ni mkubwa uliotugusa kila mmoja wetu ili kuepuka kuwakera watu kwa kufanya uzinduzi katika tarehe tuliyokuwa tumeipanga ambayo ilikuwa ni mwezi huu ambao bado tunamajonzi” alisema Amini

Baadhi ya wanamuziki wanaounda kundi hilo ni pamoja na , Mwahawa ally, Joha Kasim, Mrisho Rajab, Jumanne Ulaya, Hassan Ally, Mosi Suleiman, Rajab Kondo, Fadhili Mnara, Moshi Mtambo, Ally Kabura, Sabha, Rahma Asha Masanja na Hanifah Kasim.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...