Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, September 20, 2011

Polisi Dodoma yaitia korokoroni Moro UnitedPOLISI Dodoma, leo imetumia vizuri pingu zake, baada ya kumtia korokoroni Moro United, kwa kumchapa mabao 5-2, katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam Chamazi mjini Dar es Salaam.

Polisi Dodoma ililifikia lango la Moro United na kujipatia bao la kwanza lililofungwa na Kulwa Mobby dakika ya tano kwa shuti kali.

Bao hilo liliizindua Moro United na kuanza kulisakama lango la wapinzani wao, dakika ya 10, Fred Kahong alikosa bao baada ya shuti lake kuokolewa na kipa Aghathon Mkwandiko.

Wakicheza kwa kuelewana vizuri, Moro United walipata tena nafasi nzuri dakika ya 39, lakini Yahya Seif alishindwa kufunga bao.

Mashabmbulizi hayo yalijibiwa na Polisi Dodoma dakika ya 46, ambapo Juma Semsuya aliifungia bao la pili kwa shuti kali lililomshinda kudaka kipa wa Moro United, Steven Marashi na kujaa wavuni.

Semsuya aliiongezea bao la tatu Polisi Dodoma akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Bantu Admini.

Dakika ya 66, Semsuya aliiongezea Polisi Dodoma bao la nne likiwa la tatu katika mchezo huo akiunganisha vizuri krosi iliyotoka kwa Mobby.

Mobby aliipatia bao la tano Polisi Dodoma, lakini Moro United kupitia kwa Godfrey Wambura inajipatia bao la kwanza, na bao la pili la Moro United likafungwa na Gaudenmce Mwaikimba dakika ya 79, kwa mpira wa penalti baada ya mshambuliaji wa Moro United kuchezewa vibaya.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...