Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, September 20, 2011

STARTIMES YAZINDUA KAMPENI YA “KULA TANO”


Kampuni inayojihusisha na usambazaji wa Ving’amuzi ya Star Media(T) Limited imezindua kampeni yake mpya inayokwenda kwa jina la “KULA TANO” ambapo wateja wengi wa startimes wanatarajiwa kunufaika na kampeni hii kwa kujishindia zawadi mbalimbali.

Kampeni hii ambayo imeanza rasimi tarehe 19 septemba mpaka 31 oktoba mwaka huu itahusisha miji ya Dar es salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha, Moshi, Mbeya na Tanga. Ambapo mteja atakayenunua king’amuzi . Televisheni ya digitali ya StarTimes au kulipia miezi isiyopungua mitatu (3) atakuwa amejiingiza moja kwa moja kwenye bahati nasibu ya kujishindia hadi milioni tano (5,000,000/=) ya kitanzania.

Kampuni ya Starmedia imedhamiria kuwanufaisha wateja wake kwa kuwapa zawadi mbali mbali ikiwa na pamoja na shilingi milioni Tano kama zawadi kuu.

Pamoja na hiyo wateja wataweza kujishindia seti ya TV ya nchi 32 ambayo ni bapa au kupewa shilingi milioni moja (1,000,000/=) ya kitanzania kama udhamini wa masomo kwa wale ambao ni wanafunzi., pia watapatikana washindi ambao watajishindia Tv ya nchi 21 au kulipiwa ziara ya mapumziko itayofanyika Zanzibar kila wiki.

Vilevile watapatikana wateja saba (7) kila siku ambao watakuwa wakijishindia malipo ya miezi mitatu nakufurahia program nzuri kutoka startimes . Hivyo basi wateja wa star times na wale watakao jiunga wana fursa hii ya kujishindia zawadi mbali mbali na kufurahia mfumo huu wa digitali.

Aidha kampuni ya Star media imeongeza chaneli mpya katika king’amuzi chake cha startimes ambapo mteja sasa anaweza kufurahia chaneli ya Kungfu ambayo itakuwa ikionesha filamu za kichina na pia michuano ya soka ambayo itakuwa ikioneshwa moja kwa moja, kwa hivi sasa chaneli ya Kungfu ina onesha ligi ya Italia maarufu kama serie A. chaneli nyingine zilizo ongezwa ni Hits music, euro channel, Nature and History , MCS na Gbs. Pia kuanzia mwezi wa kumi StarTimes itakuwa ikitoa huduma zake katika kifurushi cha Mambo kitachogharimu (9000/= Tsh ) na Uhuru(18,000/=Tsh) kumpa mwanya mteja kulipia awezavyo.

Hii imekuwa ikifanyika ili kuongeza wigo wa mtumiaji wa startimes kuchagua chaneli na mambo ambayo atafurahia kuyaangalia kupitia king’amuzi chetu cha starTimes .

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...