Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, September 25, 2011

SIMBA WALIA NA WAAMUZI, WADAI UZEMBE WAO UNACHANGIA WACHEZAJI WAO KUUMIZWA


WAKATI vinara wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, Simba, wanashuka katika Uwanja wa Taifa kesho kukwaana na Mtibwa Sugar ya Morogoro, uongozi wa timu hiyo umetoa wito kwa waamuzi wa Ligi Kuu kulinda wachezaji wake.
Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa kutokuwa makini kwa waamuzi hao kumechangia kuongezeka kwa majeruhi kadiri ligi inavyokwenda mbele.
Alisema wachezaji wa timu pinzani ambazo wamekutana nazo katika ligi hiyo wamekuwa wakiwachezea vibaya wachezaji wake kabla ya kuwaumiza lakini waamuzi wamekuwa wakichukulia kama jambo la kawaida.
“Kwa kweli hali hii inatishia maendeleo ya timu yetu katika kampeni zake za kusaka ubingwa kwenye ligi hiyo, tunawaomba waamuzi kuwa makini sambamba na kuwaadhibu wachezaji wa timu pinzani ambao watajaribu kucheza rafu zisizo na maana,” alisema Kamwaga.
“Mfano ulio wazi ni wa mshambuliaji wetu Sunzu (Felix) ambaye alichezewa rafu ya makusudi na kuumia katika mechi yetu na Toto African ya Mwanza, hivyo kushonwa nyuzi nne, hata Garvies Kago aliangushwa na mmoja wa mabeki wa Toto, kabla hajaamka alikanyagwa mgongoni lakini mwamuzi hakufanya lolote,” aliongeza.
Mbali na Sunzu, majeruhi wengine katika timu hiyo ni pamoja na Amir Maftah anayesumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu na Salum Machaku aliyevunjika mguu.
“Tunaomba waamuzi watulinde na waonyeshe uungwana katika michezo ya Ligi Kuu, ili tucheze soka, kwani soka si vita, ndiyo maana wadau wengi wametoa fedha zao nyingi ili kujioea burudani hiyo,” alisema Kamwaga.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...