Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, September 14, 2011

Haye adai Lewic kampa dawa


DAVID Haye amesema ameamua kuchelewa kustaafu ngumi kutokana na kutaka kupigana na Vitali Klitschko ili kuutwaa ubingwa wake wa WBC.
Mpiganaji huyo wa London alipigwa na nduguye Vitali, Wladimir Julai awali alisema kuwa anataka kustaafu ngumi baada ya kusherekea miaka 31 ya kuzali kwake mwezi ujao.
Lakini Haye, ambaye alidai kuwa alipigana huku akiwa na maumivu kutokana na kuvunjika kidole cha mguu na kupoteza ubingwa wa WBA, amesema kuwa anataka kupiganba na Klitschko mkubwa.
Vitali mwenye miaka 40, alitetea ubingwa wake kwa kushinda katika raundi ya 10 dhidi ya mpiganaji wa Poland, Tomasz Adamek Jumamosi.
kwa mujibu wa gazeti la Mirror, Haye anataka kupigana na na mpinzani wake mwenye urefu wa futi 6 na inchi 7 raia wa Ukraine baada ya kuzungumza na bingwa wa zamani wa dunia Lennox Lewis alipokuwa Jamaica Julai mwaka huu.
Haye alisema: “Nimefikiria kila kitu baada ya kuzungumza na familia yangu na kukutana na Lennox mjini Montego Bay. Tuliuuzungumza na Lennox alinipa vitu muhimu kwa ajili ya kupiga Vitali, kama alivyofanya 2003.
“Vitali anatakwia kunipatia nafasi, kama anajisikia.”
Vitali bado ana uchungu kutokana na Haye kuvaa fulana iliyokuwa na picha inayomwonesha ameshika kicha chake na nduguye vilivyochinjwa, Jumamosi hakutaka kuzungumzia kuhusu kuwepo kwa pambano hilo kwenye uwanja waWembley.
Vitali alisema: “Haye ni mpiganaji anayeongea mambo machafu katika ngumi. Amenigusa binafsi na ninataka kumtwanga.”

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...