Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, September 20, 2011

Wacheza Dansi wa muziki wa Salsa ‘Mutati Dancers’ toka Kenya na Kundi la Tanzania House of Talent (THT) kuweka nakshi Tafrija ya Hisani ya Shear


Kwa mara ya pili mfululizo, kampuni ya Shear Illusions ya Tanzania inawaletea tafrija ya hisani ya kila mwaka ya Shear (Shear Charity Ball 2011) yenye lengo ya kutunisha mfuko na kusaidia akina mama wenye matatizo ya fistula katika hospitali ya CCBRT na pia kuwezesha ukarabati wa mfumo mzima wa maji safi na maji taka katika hospitali ya Amana zote za Mkoa wa Dar es Salaam.

Tafrija hii ya hisani itafanyika tarehe 01 Oktoba kuanzia saa moja kamili jioni katika ukumbi wa Kivukoni, uliopo katika hoteli ya Movenpick. Ticketi zote za tafrija hii zitauzwa kabla ya siku ya tafrija.

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa tafrija hiyo kufanyika. Katika tafrija iliyofanyika mwaka jana ambayo mgeni rasmi alikuwa Mbunge Wa Bumbuli, Mhe. January Makamba, kiasi cha shilingi milioni 15 kilichangwa. Nusu ya fedha hizo zilikwenda CCBRT kwa ajili ya matibabu ya akina mama wanaosumbuliwa na fistula wakati nusu ya fedha nyingine zilipelekwa kuwasaidia watoto wahitaji wanaolelewa katika vituo vya SOS jijini Dar es Salaam.

Kutokana na ukubwa wa mahitaji, katika tafrija ya mwaka huu inalenga kuchangisha shilingi milioni 50 kwa ajili ya taasisi hizo mbili, za CCBRT na hospitali ya Amana zote za Mkoa wa Dar es salaam.

Katika kufanikisha tafrija hiyo ya hisani kwa mwaka huu inayobeba ujumbe usemao; “Mimi na wewe tuungane kuleta tabasamu kwa watanzania wenzetu”, kamati ya maandalizi imewaalika wachezaji wa kimataifa wa muziki wa Salsa wanaounda kundi maarufu la Mutati Dancers wanaotoka nchini Kenya kuweka nakshi katika usiku huo wa pekee. Mbali na hao, kutakuwa na onyesho kabambe toka kwa kundi maarufu la Tanzania House Of Talent (THT) linaloshirikisha wasanii wenye vipaji vya kipekee.

Aidha tafrija hiyo itapambwa pia na muziki murua wa miaka ya 60, 70 na 80 itakayokuwa ikiporomoshwa na mmoja wa Ma-DJ mahiri miondoko ya muziki ya wakati huo, DJ Bony Love.

Tunawashukuru sana wadhamini waliojitoa kwa hali na mali katika kufanikisha tafrija hii. Shukrani za pekee ziwafikie Serengeti Breweries, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Billicanas Group, Kampuni ya kimataifa ya ulinzi ya Group 4, Shirika La Nyumba la Taifa (NHC), Fly 540, Maxcom, Precision Air, Desktop Production (DTP), Peacock Hotel, Clouds Media Group, kampuni ya vifaa vya ujenzi ya SS Concrete, benki ya Azania, Benchmark Production, Advertising Dar, SBC Tanzania (Pepsi), Tanzania House of Talent (THT), I-View Media, mafuta ya kulainisha ngozi – Cocotan, duka la nguo la Tina Maria, Kampuni ya kupamba ya Hugo Domingo, Imaging Smart na AIESEC.

Tunatoa wito kwa makampuni na watu binafsi ambao wangependa kuchangia kufanya hivyo kwani siku zilizobakia bado ni chache. Wanaweza kufanya hivyo kwa kuchangia fedha wa kwa kununua tiketi za mtu mmoja mmoja au za watu 10 zinazotolewa kwa makundi au makampuni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...