Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, September 13, 2011

Tegete apigwa stop YangaMSHAMBULIAJI wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Jerryson Tegete, amesimamishwa kuitumikia timu hiyo kwa utovu wa nidhamu alioufanya leo asubihi wakati wa mazoezi ya timu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Yanga, Louis Sendeu, amesema mshambuliaji huyo alitofautiana na Kocha Sam Timbe, wakati wa mazoezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Kaunda mjini Dar es Salaam.

Sendeu amesema kuwa, kitendo hicho kimewafanya viongozi wa klabu hiyo kumchukulia hatua za kinidhamu, wakianza kwa kumsimamisha kuitumikia timu hiyo inayosuasua katika Ligi Kuu Bara.

Yote hayo, yanaweza kuwa, yanatokea kutokana na mwenendo wa timu hiyo katika ligi kuu, kwani mpaka sasa ianshika nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi tatu baada ya kucheza mechi nne.No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...