Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, September 22, 2011

KLABU ZA NGUMI ZATAKIWA KUJIANDAA NA MICHUANO YA KAMANDA KOVA


KLABU za ngumi za mkoa wa Pwani na Dar es Salam zimetakiwa kujiandaa vema kwa ajili ya michuano ya ngumi ya kuwania kombe la Kamanda Kova 'Kova Cup' litakalowaniwa Oktoba 24 mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam , Katibu Mkuu wa Shirikisho la ngumi za ridhaa nchini (BFT), Makore Mashaga alisema klabu hizo zitakapojitokeza kwa wingi zitatoa changamoto kwa timu ya Taifa ambayo inajiandaa na mashindano mbalimbali ya Kimataifa.

"Kwa sasa mabondia wetu wanaendelea na mazoezi kama kawaida chini ya kocha mkuu Hurtado Primentel ambapo nao watashiriki michuano ya Kova Cup kwa ajili ya kujiweka sawa,"alisema Mashaga.

Alisema michuano hiyo itatoa mabondia mbalimbali kutoka mikoa ya Pwani na Dar es Salaam ambapo watashiriki kama klabu huku kila moja ikiwania kombe hilo ambalo limeandaliwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Suleiman Kova.

Timu hiyo ya Taifa inafanya mazoezi yake katika uwanja wa ndani wa Tafa Dar es Salaam tangu iliporejea nchini kutokea Maputo Msumbiji ilipokuwa ikishiriki Michuano ya Mataifa ya Afrika.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...