Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, September 22, 2011

SUPER D , KINYOGOLI WATAMBA BONDIA WAO KUFANYA VIZURI


KOCHA wa bondia Yohana Robart, Rajabu Mhamila 'Super D' ametamba bondia wake kuibuka na ushindi katika pambano lake dhidi ya bondia Mohamed Ndonga litakalofanyika JUMAMOSI katika ukumbi wa DDC Magomeni.

Pambano hilo ni la maandalizi kwa bondia huyo kutetea mkanda wake wa Oganaizesheni ya Ngumi za KUlipwa (TPBO) litakalofanyika jijini Tanga Septemba 30 mwaka huu ambapo atapambana na Alan Kamote wa jijini Tanga.

Akizungumzia maandalizi ya bondia huyo Super D alisema maandalizi ya bondia huyo ni mazuri na anafanya mazoezi chini ya kambi ya ngumi ya Kinyogoli Foundation.

"Nategemea bondia wangu kuibuka na ushindi katika pambano lake la Septemba la jumamosi, ambalo kwa kiasi kikubwa litamsaidia katika maandalizi yake katika pambano la Tanga ambalo litakuwa la raundi 10,"alisema Super D.

Alisema bondia huyo atapigania uzito wa kg. 60 light weight ambapo katika pambano lake la kesho atapigana raundi sita.

Seper D alisema mapambano hayo ni moja ya muendelezo wa kuendeleza vipaji vya mabondia mbalimbali ambapo amewaomba wadau kujitokeza ili kusaidia juhudi hizo zinazofanywa na kambi ya ngumi ya Ilala.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...