Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, September 16, 2011

BONDIA KALAMA NYILAWILA ATAFUTA PROMOTA KWA AJILI YA KUPAMBANA NA CHEKABONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Kalama Nyilawila amesema kwa sasa ameanza mchakato wa kutafuta promota kwa ajili ya kumuandalia pambano dhidi ya francis Cheka ili aweze kutetea ubiungwa wake wa WBO.

Akizungumza na majira jana, Kalama alisema, kutokana na malengo yake ya kutaka mkanda huo ubaki hapa nchini hivyo alionelea kucheza na Cheka kutokana na kuwa na uwezo mkubwa na hasa mchezo mzuri aliouonyesha katika pambano lao la marudiano dhidi yake na Mada Maugo kwa kumtandika na kumzidi tofauti ya pointi.

Alisema, kwa sasa ameishaanza kusaka promota ambapo bado wapo katika mazungumzo ya awali ambapo watakapoa afikiana ndipo watapanga tarehe halisi ya kufanya pambano hilo ikiwa ni pamoja na mahali.
"Kama nilivyosema sitaki mkanda huu utoke nje hivyo nikifanikiwa kucheza na Cheka itakuwa faraja kwangu kwani najua uwezo wake na hata anatambulika Duniani hivyo haitakuwa vibaya kwani naye alishawahi kucheza mapambano ya Kimataifa," alisema Kalama.
Aliongeza kuwa wakati wa yeye kutetea ubingwa huo umefika ambapo akishindwa kucheza na bondia wa hapa nchini anatakiwa kutafuta pambano la nje ya nchi ili kuweza kutetea ubingwa huo kiyu ambacho yeye hakitaki lakini ikishindikana kupata pambano hilo itabidi atafute pambano la nje.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...