Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, October 22, 2010

ALLY CHOKI KUITEKA MOSHI ARUSHA NOVEMBA 19 NA 20


BENDI ya muziki ya Extra Bongo inatarajia kwenda kufanya maonesho mawili makubwa katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha yatakayofanyika Novemba 19 na 20 katika mikoa hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi wa bendi hiyo Ali Choki alisema wameamua kufanya maonesho katika mikoa hiyo ili kuwapa burudani wakazi wake ikiwa ni mwendelezo wa maonesho waliyopanga kuwapa wakazi wa mikoa ya kaskazini.

Alisema onesho la kwanza watafanya mkoani Kilimanjaro katika ukumbi wa Adventure novemba 19 na Arusha novemba 20 litafanyika Matongee klabu.

Alisema maonesho hayo yatawapa fursa ya kuitangaza albamu yao ya Mjini Mipango na staili yao mpya ya uchezaji inayofahamika kama 'Kizigo' ambayo imekuwa ikiwavutia na wengi tangu ilipoanzisho.

"Tunashukuru kuona maonesho mengi tunayoyafanya mashabiki wetu wanatuunga mkono kwa kiasi kikubwa na sisi tunaendelea kuleta vitu vipya na sasa tunakwenda Arusha ambako tutafanya onesho moja na Kilimanjaro moja.," alisema Choki.

Choki ambaye pia ni mwimbaji wa bendi hiyo alisema maonesho hayo yatakuwa ni ya kukata na soka kutokana na kuwa onesho la kwanza la bendi hiyo tangu ilipoanzishwa kwa mara nyingine.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...