Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, October 27, 2010

PWEZA PAUL AFARIKI DUNIA KUJENGEWA MNARA ATAKAPOZIKWA


PWEZA aitwaye Paul aliyejizolea umaarufu wakati wa michuano ya kombe la Dunia Afrika Kusini 2010 kwa kutabiri matokeo kwa uhakika, amekufa jana asubuhi na kuelezwa kuwa amekufa kifo cha kawaida.

Wakati wa mashindano ya Dombe la Dunia alikuwa akitimiwa kwa utabiri kwa kumwekea mkebe ulikuwa na chakula chake na bendera za nchi ambapo, mahali alipoenda ndipo ilipewa nafasi na kushinda, na ilikuwa hivyo.

Pweza huyo alikufa akiwa katika katika kituo cha Oberhause, Ujerumani ambapo alikuwa akihifadhiwa. Kifo cha pweza huyo kimewasikitisha mashabiki wa soka wa Ujerumani na sehemu mbalimbali duniani.

"Tumesikitishwa kwa kujua kuwa alifurahia maisha mzuri hapa," alisema Stefan Porwoll, meneja wa kituo cha Oberhausen Sea Life Center kilichopo magharibi mwa Ujerumani. Alikuwa akikuwa akikua kawaida na tutamkosa sana."

"Paul aliishangaza dunia kwa kutabiri kwa usahihi wakati wa mapambano ya Ujerumani na kisha kutabiri fainalil," Porwoll alisema,kwa mujibu wa CNN.

Kituo hicho kinapanga taratibu za mazishi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...