Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, October 20, 2010

MAONESHO YA Swahili Fashion Week KUANZO NOVEMBER 4


Kwa mara ya tatu sasa Swahili Fashion Week itafanyika Karimjee Hall kuanzi tarehe 4 hadi 6 November 2010, Dar Es Salaam , Tanzania .


Swahili Fashion Week itawaleta pamoja wabunifu wa mavazi 24 kutoka nchi zinazoongea lugha ya Kiswahili ili kuweza kuonyesha ubunifu wao katika kubuni mavazi ya aina mbalimbali kwa kutumia aina mbalimbali za malighafi.


Wabunifu watakaoonesha mavazi katika Swahili Fashion Week kwa mwaka huu ni pamoja na Ailinda Sawe, Manju Msita, Kemi Kalikawe, Christine Mhando, Shellina Ibrahim, Farha Naaz Sultan, Gabriel Mollel, Robi Morro, Asia Idarous, Zamda George, Khadija Mwanamboka, Jamilla Vera Swai and Made by Afrika. wabunifu kutoka Kenya ni Sonu Sharma, Moo Cow, KiKoromeo, John Kavike na Kooroo, na kutoka Uganda ni mbunifu Stella Atal.


“Pamoja na maonyesho ya mavazi, mwaka huu Swahili Fashion Week itakwenda sambamba na tamasha la maonyesho ya bidhaa mbalimbali zenye asili ya mswahili kutoka mwambao wa Afrika mashariki”. Alisema Mustafa Hassanali muaandaaji y tukio la Swahili Fashion Week.


“Tunafungua milango zaidi kwa ajili ya watazamaji wapya wa Swahili Fashion Week, amboa watapata fursa ya kununua bidhaa mbalimbali. Tamasha hili ambalo linazileta pamoja bidhaa mbalimbali za sanaa na utamaduni wa mswahili, pia litahamasisha ubunifu zaidi katika bidhaa zinazokwenda sambamba na maisha halisi ya jamii ya watu wanaoongea lugha ya Kiswahili kwa kukutana pamoja na kubadilisha mawazo na kujifunza uzoefu mpya katika masuala yanayohusiana na sanaa kwa ujumla.” Aliaongeza Hassanali.


Pamoja na maonyesho, pia kutakuwepo aina tofauti za burudani kutoka kwa vikundi


Mbalimbali vya muziki, uchoraji wa hina, usukaji mikeka, sambamba na semina za aina tofauti zitakazo washirikisha wabunifu wa mavazi.


Aidha Swahili fashion Week imeandaa aina tofauti za zawadi zitakazotolewa mwaka huu kwa lengo la kutambua na kuthamini vipaji vya aina mbalimbali vitakavyooneshwa, ikiwa ni pamoja na zawadi ya mwaka kwa mbunifu anaechipukia.


Swahili fashion week 2010 imedhaminiwa na Home of Swahili Fashion week Southern Sun, Origin Africa, USAID Compete, EATV, East Africa Radio, Malaria Haikubaliki, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) Ultimate Security, Monier 2000, Colour Print ltd, Global Outdoor Ltd, Amarula, Vayle Springs Ltd, ZG Films, Darling Hair, Danish make up designs, Nipashe, Bilicanas, Perfect Machinery LTD, 1 & 1 internet solutions, Sengi Tours, Ifashion na 361 Degrees.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...