Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, October 12, 2010

KAIJAGE ATOLEWA KAFARA TFF


SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limemsimamisha kwa muda wa mwezi mmoja, Ofisa Habari wake Florian Kaijage baada ya tukio la kutoimbwa kwa nyimbo za Taifa katika mchezo kati ya timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars na Morocco katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki kombe la Mataifa ya Afrika.

Siku ya Jumamosi , tarehe 9 Oktoba 2010, tumeshuhudia fedheha ya kushindwa kutimiza itifaki muhimu ya kupiga nyimbo za taifa husika, yaani nyimbo ya taifa ya Morocco na nyimbo ya taifa ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Hilo lilikuwa ni tukio la aibu sana kwa nchi yetulililofanyika mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania , Mhe Jakaya Mrisho Kikwete , mbele ya halaiki ya wapenzi wa mpira wakiwemo wageni wetu wakiongozwa na Balozi wao.Lakini pia , kwa vile mchezo huo ulionyeshwa katika luninga ndani na nje ya nchi , tukio hili la aibu limeshuhudiwa pia na Watanzania nchini kote na wapenzi wa mpira duniani.

Jambo la kusikitisha ni kuwa tukio hilo halikustahili kutokea.Kwa kuwa tatizo la nyimbo za taifa kutopigwa ipasavyo katika michezo ya kimataifa lilishawahi kutokea .Jitihada mahsusi zilizfanywa kuhakikisha kuwa safari hii jambo hili halitokei.Wahusika walipewa jukumu la kuhakikisha kuwa wanazijaribu nyimbo hizo siku mbili kabla ya mchezo na kuhakikisha kuwa hakuna hitilafu yeyote itakayotokea.Wahusika walifuatiliwa kwa karibu na kila walipoulizwa walikuwa wakijibu kuwa wamesha hakikisha kuwa hakutatokea dosari yeyote.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...