Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, October 23, 2010

MASENETA WA MSONDO WAKUTANA KUPANGA MIKAKATI YA BENDI HIYO


MASENETA wa Bendi ya Msondo Mgoma jana wamekunatana kujadili mstakabari mzima wa bendi hiyo ilipo sasa na inapoelekea tangu kifo cha Moshi William TX..

Masenata hawo walikutana katika mkutano uliofanyika kwenye makao makuu ya ya bendi hiyo Amana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila (Super D) alisema kuwa kati ya ajenda waliojadili ni pamoaja na mwenendo mzima wa bendi hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa inazidi kupoteza mashabiki.

Alisema pamoja na hilo pia walijadili jinsi watavyo anza kuifufua upya bendi hiyo na kuongeza wasanii wawili wapya ili kuongeza nguvu katika kutoa burudan.

"Sasa bendi yetu haipo kama zamani hivyo tunakaa vikao kujadili ni namna gani tutakavyoweza kuitengeneza upya bendi yetu ikiwa na kuongeza wasanii wengine wapya ambao tunaimani watareta nguvu ndani ya bendi yetu," alisema Super D.

Pia alisema baada kikao hicho wanatarajia kukutana tena Novemba 5 mwaka huu ili kuwatangaza wasanii wapya ambao watatoka ndani ya bendi za jijini Dar es Salaam.

Alisema tangu alipofariki Moshi Williamu TX bendi hiyo imekuwa na muelekeo mbaya ambapo ndiyo mtu aliyekuwa tengemezi kubwa ndani ya bendi hiyo ambayo ilijipatia umaarufu mkubwa miaka ya nyuma na kuleta tunzo 4 mfululizo ndani ya miaka hiyo ikiwemo Kilimanjaro Music Awards.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...