Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, October 20, 2010

ZANTEL YAKABIDHI MILIONI MILIONI KWA WATU WATATU LEO


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zantel leo, imekabidhi zawadi za sh. milioni 1 kwa washindi wengine watatu wa droo ya 'Hamisi Ma SMS'.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano Dar es Salaam jana, Meneja Mauzo wa Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Edgar Mapande alisema hadi kufikia jana jumla ya wateja 16 walimeshinda na kukabidhiwa zawadi zao.

Alisema kati ya washindi hao, nane wanatoka Tanzania Visiwani huku wengine nane wakitoka Tanzania bara.

Bw.Mapande aliwataka wateja wa Zantel kuendelea kucheza droo hiyo ili waweze kujishindia zawadi.

"Nawapongeza wateja mliobahatika kushinda nawaomba wateja wetu waendelee kushiriki bahati nasibu hii ili waendelee kujishindia zawadi za kila siku na za mwezi," alisema.

Wateja waliokabidhiwa zawadu zao ni pamoja na Bw. Venant Alex, Mbagala, Patrict Cyprian, Mbezi Beach, Bw. Mwatuka Sammy, Wazo Hill.

Jinsi ya kushiriki promosheni hiyo unatuma neno HAMISI kwenda namba 15587 kwa gharama ya sh. 350 kwa kila ujumbe.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...