Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, October 24, 2010

NCCR MAGEUZI YAPINGE NEC KUTOWALIPA POSHO MAWAKALA


CHAMA cha NCCR Mageuzi kimesema kinapokea kwa masikitiko taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa haitawajibika kuwalipa ama kuwapa posho mawakala wa Vyama vya Siasa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam mkuu wa idara ya kampeni na uchaguzi ya chama hicho Bw.Faustin Sungura alisema NEC ina wajibu wa kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria za uchaguzi pamoja na sheria nyingine za nchi.

Bw.Sungura alisema Julai 26 mwaka huu NEC chini ya Jaji mstaafu Bw.Lewis Makame ilisaini kuheshimu kutii na kutekeleza maadili ya uchaguzi pamoja na wajibu wake.

"Ndugu waandishi wa habari,vifungu 92 (1) cha sheria na 4 (1979) ya uchaguzi wa madiwani ,pamoja na kifungu cha 93 (1) na (2) cha sheria na 1(1985) ya uchaguzi wa wabunge na Rais vinawataka mawakala wote wa vyama vya siasa kabla ya kuanza kazi ya kusimamia au kuangalia mchakato mzima wa kupiga kura kuhesabu na kutangaza matokeo,kula kiapo cha kutunza siri "alisema

Anaongeza "Aidha watendaji wote wanaosimamia uchanguzi chini ya NEC hutakiwa kwanza kula kiapo cha kutunza siri za uchaguzi na wote hawa wanalipwa posho bila kujali kama wanalipwa mishahara au la!,ni wazi kuwa watu hawa wamekuwa sehhemu ya uchaguzi "alisema

Bw.Sungura anasema serikali haiwezi kumpa mtu kazi ya kufanya bila kumlipa na hasa inapokuwa nyeti na inayomlazimu mtu huyo kula kiapo kwanza.

Hata hvyo amewaomba wapiga kura kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kupeleka madiwani wengi kwenye halmashauri za Wilaya ,miji na Manispaa na wabunge wengi kutoka upinzani.

Akizungumzia kusimamisha mgombea mmoja wa kambi ya upinzani wa nafasi ya Urais alisema vyama vya upinzani vimekubaliana kujipa mda ili kuimarisha nguvu ya upinzani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...