Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, October 23, 2010

CCM YATOA ZAWADI KWA WASHINDI


WASHIRIKI tisa wa Bahati Nasibu ya Changia Chama cha Mapinduzi (CCM), wamezawadiwa zawadi zao katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya chama hicho, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Mjumbe wa Halmashauri ya CCM Taifa, Asha Baraka, alisema Mtanzania yeyote anaruhusiwa kucheza bahati nasibu huyo.

Asha alisema CCM haina ubaguzi, hivyo mwanachama wa chama chochote anaruhusiwa kucheza bahati nasibu hiyo, na ikiwa atashinda atakabidhiwa zawadi yake kama kawaida.

¡°CCM hatuna ubaguzi, milango iko wazi kwa kila mtu, hata awe wa chama kingine, akishinda tutamkabidhi zawadi yake kama kawaida,¡± alisema.

Aliwataja walioshinda pikipiki ni Paul Wanyama na Deus Makua, wakati John Mfomoka, alishinda zawadi ya baiskeli.

Wengine waliojinyakulia kitita cha sh. 100,000 kila mmoja ni Nice Kisunte, Leah Pascal, Sama Rashid, Juma saleh, Sunday Mchunga na Joshua Alloyce.

Asha alisema walioshinda walituma ujumbe wa kuichangia CCM na namba zao kuingizwa kwenye bahati nasibu hiyo.

¡°Hawa walituma ujumbe wa kuchangia CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu, namba zao zikaingizwa kwenye bahati nasibu, wameibuka na pikipiki,alisema.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...