Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, October 14, 2010

MCHAMBUZI WA SOKA AIBUKA NA MILIONI KUMI ZA SUPA PESA


Msemaji mkuu wa Supa Pesa Natasha Issa akimkabidhi hundi mshindi wa milioni kumi Dr. Licky Abdallah


MSHINDI WA TATU WA MILIONI KUMI ZA SUPA PESA APATIKANA!

Mshindi wa tatu wa Milioni Kumi, Dr. Licky Abdallah mwenye umri wa miaka 52, wa bahati nasibu ya kipekee ya SUPA PESA amekabidhiwa hundi ya fedha hizo jana jijini Dar es salaam.

Dr. Licky Abdallah ambaye ni mkazi wa Dar es Salaam, ni mkurugenzi wa kampuni ya Malagarasi Tours and Safaris na pia ni mchambuzi maarufu wa wa mpira wa mguu (soka ) hapa jijini. Alipokea hundi hiyo kwa furaha na kusema kwamba alikuwa akichukulia kama utani pale ambapo alisikia kuhusu droo hii ya Supa Pesa na kushiriki kama utani.

‘Ilitokea kama bahati kubwa pale ambapo nilipigiwa simu na kituo cha radio Clouds FM kujulishwa kuhusu ushindi wangu. Kiukweli nilijawa na furaha sana. Pesa hizi nitaziongezea kwenye mtaji wa biashara yangu na pia kumtunuku zawadi binti yangu ambaye alinishawishi kushiriki droo hii ya Supa Pesa.’ Alisema Dr. Licky.

Msemaji wa Supa Pesa, Bi. Natasha Issa, kwenye zoezi la kumkabidhi mshindi huyo hundi yake,
amesema kwamba washindi wanazidi kumiminika kila siku kutoka kila kona ya Tanzania. Aliwataka watanzania wengi zaidi kushiriki droo hii ambapo kila siku kunapatikana washindi watatu wa milioni moja, na Mshindi mmoja wa Milioni Kumi kila wiki.

Bi. INatasha aliongezea kwa kusema,‘Kushiriki droo ya Supa Pesa ni rahisi, inahitaji kutuma ujumbe mfupi wenye neno SUPA kwenda namba 15777. Hii inakuwezesha wewe kuingia moja kwa moja kwenye ushindani wa shilingi milioni moja kila sikui na ukishiriki kutuma Ujumbe mfupi wa simu zaidi ya mara nne basi utakuwa kati ya washindani wa milioni kumi kila wiki,’

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...