Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, October 21, 2010

SUPA PESA YAMTOA GRECE


Msambazaji wa vifaa vya ofisini na shuleni, Bi. Grace Absalom, amebahatika kuwa kati ya washindi waliojinyakulia Milioni Kumi kupitia bahati nasibu ya simu za mkononi, Supa Pesa.

Katika hafla ya kukabidhiwa hundi, Mshindi huyo alisisitiza kuwa alipata mshtuko kiasi cha kupata wasiwasi alipopata simu ya kutaarifiwa ushindi wake,kana kwamba sio ukweli yale aliyokuwa akiambiwa. ‘ Nilipata shauku sana hasa baada ya kupata simu niliyopigiwa na mtangazaji wa redio kunijulisha kuhusu ushindi wangu. Sikuamini kabisa niliyoyasikia, niliona kama ni utani mpaka kufikia kumuuliza mtangazaji huyo mara mbili mbili kuhakikisha sio utapeli.

Namshukuru Mungu ikatokea ni ukweli nilipata ushindi wa
Supa Pesa na papo hapo nikajawa na furaha sana.’ alisema Grace.Grace alipokea hundi yake ya milioni Kumi katika ofisi za Supa Pesa jijini Dar es Salaam, mbele ya waandsihi wa habari pamoja na mwakilishi kutoka bahati nasibu ya taifa, Bw. Abdallah Salim. Meneja mkuu wa Supa Pesa,Bi. Natasha Issa, akiwa anamkabidhi Bi. Grace hundi lake alisema, Supa Pesa inazidi kubadilisha maisha ya watanzania wanaoshiriki droo hiyo.

‘Ni jambo la faraja sana punde anaposhinda mshiriki wa droo hii rahisi ya Supa Pesa ,na kupata ushuhuda jinsi maisha yanavyobadilishwa siku baada ya siku kupitia bahati nasibu hii hasa kwa fedha wanazopata washindi. Tunazidi kuwahamasisha washiriki wetu watume ujumbe mfupi wenye neno SUPA kuenda namba 15777 zaidi na zaidi ili kujiongezea nafasi za ushindi kila siku. Supa Pesa inatoa fedha taslimu Milioni Moja kwa washindi wa tatu kila siku na Milioni Kumi kwa mshindi anayeshiriki kutuma ujumbe mfupi zaidi ya mara nne kwa wiki.’

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...